Taasisi
ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania watapakaa mkoani Dodoma
kunusa harufu ya rushwa inayonukia kwa wapambe wa makada wanaongoja
kuchujwa usiku wa leo.Taasisi hiyo imetapakaa kila kona ili kuwabana
wote watakao sadikika kuchukua au kugawa bakishishi hiyo ili kupigiwa
kura kinyume na taratibu na kanuni za chama na nchi.
Ijumaa, 10 Julai 2015
Alhamisi, 9 Julai 2015
Rose Muhando ''Nafikiri Kurudia Kwenye Uislamu''
Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
NYOTA wa
nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema
alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo
zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi
katika imani yake ya kwanza.Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.
Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.
“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.
“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.
Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.
Rais Kikwete Aonesha Imani Yake Kwa Lowasa.
BUNGE LALIPUKA KWA SHANGWE.
Katika
hotuba ya rais jioni ya leo amemshukuru waziri mstahafu Edward Lowasa
kwakumsaidia katika uongozi wake.Ndipo Bunge Likalipuka Kwa Shagwe Wakimshangilia Mgombea Huyo Wa Urais.
Edward Lowasa Kwa Heshima Na Tahadhima Akainuka Kuonesha Heshima Kwa Rais Na Wabunge Kwa Kutambua Mchango Wake Kwenye Uongozi Wa Awamu Ya Nne.
Alhamisi, 2 Julai 2015
Breaking News..!!! Chadema Wakamatwa Na Mashine Ya BVR Wakiandikisha Watu Usiku Na Kuwalipa Huko Wilayani Kahama
Jeshi la polisi wilayani
kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika
kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa
wa Nyakato wilayani humo Mayunga Alphonce kupitia CHEDEMA.
Akizungumza leo na
waandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amesema tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika mtaa wa nyakato ambapo
mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura.
Mpesya amesema kuwa
vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema
ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho
vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.
Ameongeza katika
harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu
mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine
hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo wa mtaa.
Mpesya amesema jeshi la
Polisi wilayani humo linamshikilia kaimu afisa mtendaji wa kata ya
Nyasubi Lugina Misango ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine
hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa myekiti wa
mtaa.
Katika hatua nyingine
Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo,
kutambua kuwa ofisi yake ni mamlaka kamili ya serikali na kwamba
wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo
upo kituo cha polisi.
Tangu kuanza kwa zoezi
la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura
wilayani humo hilo ndio tukio la kwanza la aina yake ambalo limevuta
hisia, na Mpesya amesema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi.
Breakin Newzz!!!:- Msumbiji Wahalalisha Ndoa Za Jinsia Moja Live!!!
Ajali..!!! Watano Wapoteza Maisha Baada Ya Magari Mawili Kugongana Huko Bukombe, Geita
Watu 5 wamefariki dunia
papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita
mara baada ya magari mawili kugonganana uso kwa uso katika kijiji cha
Ishororo kata Bukombe mkoani humo.
Ajali hiyo imetokea jana
majira ya saa 12 jioni ikihusisha magari mawili aina ya Toyota yenye
namba T-302-DDT na T-402-CQJ, huku chanzo kikidaiwa kuwa mwendokasi
uliosababisha madereva hao kushindwa kuchukua tahadhari.
Mganga mkuu wa hospitali
ya wilaya wa Bukombe Mkoani Geita Dk. Daniel Sulusi amethibitisha
kupokea maiti 5 na majeruhi watatu ambao amesema hali zao ni mbaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo
wamesema kuwa endapo madereva hao wangekuwa
wanaendesha magari hayo mwendo wa kawaida wangeweza kuepusha ajali hiyo
kwani eneo hilo linapitika vizuri na halina kikwazo chochote.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)