Social Icons

Jumapili, 10 Mei 2015

Wanafunzi wa Kozi ya Mafunzo ya Upigaji wa Picha na Photoshop Wamuaga Mkufunzi wao kutoka JICA Japan

 

Ofisa  Muandamizi wa Idara ya Habari Maelezo  Zanzibar Ndg. Faki Mjaka  akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumuaga Mtaalam wa Mafunzo ya Upigaji Picha kutoka Japan Mr Hiro, iliyotayarishwa na Wanafunzi hao na kumzawadia zawadi mbalimbali wakati wa hafla hiyo.

 Mr. Hiro Mtaalam wa mafunmzo ya Upigaji wa Picha za Mnato kutoka Shirika la Kujitolea la Japani (JICA) akiwa  makini akimsikiliza Ofisa wa Maelezo Zanzibar akitowa shukrani kwa mkufunzi hiyo, wakati wa hafla iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kipangani Café Nungwi Zanzibar.

 Mr.Hiro Matsuda akizungumza na Wanafunzi wake wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Kipangani Cafe Nungwi Zanzibar, akitowa shukrani kwa wanafunzi hao wakati wote wa mafunzo yake yaliyochukua miaka miwili ya masomo  

Wanafunzi wa Kozi ya Upigaji Picha wakimsikiliza Mr Hiro akitowa  nasaha zake kwa Wanafunzi wake baada ya kumuandalia  hafla maalum ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kipangani Café Nungwi Zanzibar.

 Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo ya Upigaji Picha kwa Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za Serikali na Binafsi wakimsikiliza Mr Hiro Matsuda.

  Mmoja wa Wanafunzi wa Kozi ya Upigaji wa Picha kutoka Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Bi Fatma, akimkabidhi kasha  ikiwa ni zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa Darasa hilo, Mr Hiroi Matsuda amemaliza muda wake Zanzibar baada ya kutoa mafunzo kwa muda wa miaka miwili. Mwanafunzi wa Darasa la Mr Hiro Matsuda Ndg Shibli Haji Shibli akimkabidhi zawadi ya fulana yenye ujumbe  Hakuna Matata Zanzibar, zawadi hizo zimetolewa na Wanafunzi wa Kozi hiyo.

 Mwanafunzi wa Darasa la Mr Hiro Matsuda Bi Miza Omar akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar zawadi hizo zimetolewa na Wanafunzi wa Kozi hiyo.

 Ofisa  Muandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar na Msemaji wa Timu ya Shaba Wazee wa Dago Ndg Faki Mjaka akimkabidhi Mr Hiro Matsuda, ikiwa ni kumbukumbu yake kutoka katika Uongozi wa timu hiyo, Mr. Hiro amebuni Nembo ya Timu hiyo ikiwa katika fulana hiyo na inatumiwa na timu hiyo rasmin kwa sasa.

 Wanafunzi wa darasa la Mr Hiro la Upigaji Picha  wakiwa katika ufukwe wa nungwi kwa ajili ya kumuaga mwalimu wao baada ya kumaliza mafunzo ya Upigaji wa Picha na Photoshop, yaliYochukua miaka miwili .

 Wanafunzi wa Kozi ya Upigaji picha na Photoshop wakifurahia wakiwa katika ufukwe wa Nungwi.

 Mr. Hiro katika pozi maeneo ya jabali la hoteli ya Nungwi akiwa na Mwanafunzi wake Othman. Wakiwa katika picha ya kumbukumbu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni