Kila mtu anapenda zawadi nzuri.. kumbukumbu nzuri ambayo atakuwa nayo staa ambae ni mmoja ya members wa Yamoto Band, Aslay ni hii gari ambayo kapewa kama zawadi ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Mkubwa Fella, ambaye ni boss wa Mkubwa na Wanawe amesema hii ni sehemu ya shukrani pia kwa Aslay ambae amekuwa nae kwa muda mrefu kwenye safari muziki.
Saidi Fella>>“Kiukweli
nina story ndefu sana kwa kijana wangu Aslay kwani nimeanza naye kazi
toka akiwa mdogo sana na amekuwa mfano wa kuigwa hata kwa vijana wenzie
nilionao katika kundi la Mkubwa na Wanawe>>
Licha ya
kumkabidhi gari leo ila bado nimewaandalia nyumba nzuri za kisasa kwa
wote wa nne na ni matarajio yangu Mheshimiwa Rais atakuja kuzindua
nyumba hizo“>> Mkubwa Fella.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni