Wahitimu wa kidato cha sita Shule ya Sekondari Kabanga iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa katika mahafali yao ya tano katika shule hiyo yaliyohusisha wahitimu 96 ambapo katika risala yao kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw. Costantine Kanyasu,walibainisha kuwa Upungufu wa mabweni ,vitabu vya kiada na ziada pamoja na walimu wa sayansi ni baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi wa shule hiyo katika mazingira ya kujifunzia
Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw Costantine Kanyasu akigawa vyeti kwa
wahitimu wa kidato cha sita ,katika shule ya sekondari Kabanga ambapo pamoja na
mambo mengine amewataka watendaji wa vijiji na kata kuwakamata wazazi na walezi
kisha kuwafikisha mahakamani wanaopuuzia kulipa karo na michango katika shule
za sekondari na ukamataji wa wazazi hao uwe sambamba na wanafunzi walioacha
shule kwa sababu tu za utoro bila kuwa na sababu za msingi kama sio utovu wa
nidhamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni