MSIMAMO VPL 2014/2015.
Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC, hapo kesho Ijumaa April 24, 2015 wanaingia
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting wakijua ushindi wa
Mechi hiyo na mwingine hapo Jumatatu dhidi ya Polisi Moro utawapa Ubingwa msimu huu huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.
Hivi sasa Yanga SC wako kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22
wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 22 na Simba SC
wapo Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 23.
Hivyo Yanga SC , ambao tayari wameshakuwa moja ya Timu mbili
zitakazocheza Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika Msimu ujao, wanahitaji
Pointi 6 tu kuwa bila Bingwa bila kujali nini mpinzani wake Azam FC anakifanya.
Azam FC Jumamosi April 25, 2015 wanacheza Nyumbani kwao na Stand United
na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu
kitu ambacho pia kitawasaidia kukwepa Simba, ambao Jumatano waliitwanga Mgambo
JKT 4-0, kuwapiku Nafasi ya Pili.
LIGI KUU VODACOM 2014/2015 RATIBA.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni