Watu 5 wamefariki dunia
papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita
mara baada ya magari mawili kugonganana uso kwa uso katika kijiji cha
Ishororo kata Bukombe mkoani humo.
Ajali hiyo imetokea jana
majira ya saa 12 jioni ikihusisha magari mawili aina ya Toyota yenye
namba T-302-DDT na T-402-CQJ, huku chanzo kikidaiwa kuwa mwendokasi
uliosababisha madereva hao kushindwa kuchukua tahadhari.
Mganga mkuu wa hospitali
ya wilaya wa Bukombe Mkoani Geita Dk. Daniel Sulusi amethibitisha
kupokea maiti 5 na majeruhi watatu ambao amesema hali zao ni mbaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo
wamesema kuwa endapo madereva hao wangekuwa
wanaendesha magari hayo mwendo wa kawaida wangeweza kuepusha ajali hiyo
kwani eneo hilo linapitika vizuri na halina kikwazo chochote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni