Taasisi
ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania watapakaa mkoani Dodoma
kunusa harufu ya rushwa inayonukia kwa wapambe wa makada wanaongoja
kuchujwa usiku wa leo.Taasisi hiyo imetapakaa kila kona ili kuwabana
wote watakao sadikika kuchukua au kugawa bakishishi hiyo ili kupigiwa
kura kinyume na taratibu na kanuni za chama na nchi.
Ijumaa, 10 Julai 2015
Alhamisi, 9 Julai 2015
Rose Muhando ''Nafikiri Kurudia Kwenye Uislamu''
Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
NYOTA wa
nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema
alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo
zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi
katika imani yake ya kwanza.Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.
Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.
“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.
“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.
Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.
Rais Kikwete Aonesha Imani Yake Kwa Lowasa.
BUNGE LALIPUKA KWA SHANGWE.
Katika
hotuba ya rais jioni ya leo amemshukuru waziri mstahafu Edward Lowasa
kwakumsaidia katika uongozi wake.Ndipo Bunge Likalipuka Kwa Shagwe Wakimshangilia Mgombea Huyo Wa Urais.
Edward Lowasa Kwa Heshima Na Tahadhima Akainuka Kuonesha Heshima Kwa Rais Na Wabunge Kwa Kutambua Mchango Wake Kwenye Uongozi Wa Awamu Ya Nne.
Alhamisi, 2 Julai 2015
Breaking News..!!! Chadema Wakamatwa Na Mashine Ya BVR Wakiandikisha Watu Usiku Na Kuwalipa Huko Wilayani Kahama
Jeshi la polisi wilayani
kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika
kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa
wa Nyakato wilayani humo Mayunga Alphonce kupitia CHEDEMA.
Akizungumza leo na
waandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya amesema tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika mtaa wa nyakato ambapo
mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura.
Mpesya amesema kuwa
vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema
ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho
vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.
Ameongeza katika
harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu
mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine
hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo wa mtaa.
Mpesya amesema jeshi la
Polisi wilayani humo linamshikilia kaimu afisa mtendaji wa kata ya
Nyasubi Lugina Misango ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine
hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa myekiti wa
mtaa.
Katika hatua nyingine
Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo,
kutambua kuwa ofisi yake ni mamlaka kamili ya serikali na kwamba
wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo
upo kituo cha polisi.
Tangu kuanza kwa zoezi
la uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura
wilayani humo hilo ndio tukio la kwanza la aina yake ambalo limevuta
hisia, na Mpesya amesema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi.
Breakin Newzz!!!:- Msumbiji Wahalalisha Ndoa Za Jinsia Moja Live!!!
Ajali..!!! Watano Wapoteza Maisha Baada Ya Magari Mawili Kugongana Huko Bukombe, Geita
Watu 5 wamefariki dunia
papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita
mara baada ya magari mawili kugonganana uso kwa uso katika kijiji cha
Ishororo kata Bukombe mkoani humo.
Ajali hiyo imetokea jana
majira ya saa 12 jioni ikihusisha magari mawili aina ya Toyota yenye
namba T-302-DDT na T-402-CQJ, huku chanzo kikidaiwa kuwa mwendokasi
uliosababisha madereva hao kushindwa kuchukua tahadhari.
Mganga mkuu wa hospitali
ya wilaya wa Bukombe Mkoani Geita Dk. Daniel Sulusi amethibitisha
kupokea maiti 5 na majeruhi watatu ambao amesema hali zao ni mbaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo
wamesema kuwa endapo madereva hao wangekuwa
wanaendesha magari hayo mwendo wa kawaida wangeweza kuepusha ajali hiyo
kwani eneo hilo linapitika vizuri na halina kikwazo chochote.
Jumamosi, 27 Juni 2015
Huzuni Yatanda Dar,Mbowe,DK Slaa Waungana Na Wanahabari Kuaga Mwili Wa Edson Kamukara.
Pichani
ni mkurugenzi wa magazeti ya halisi piblisher na mwandishi nguli wa
habari za uchunguzi tanzania SAID KUBENEA akiuaga mwili wa mfanyakazi
mwenzake EDSON KAMUKARA LEO Jijini Dar es salaam
Aliyekuwa
mwandishi wa habari wa magazeti ya hali halisi publisher wazalishaji wa
gazeti la mawio na mwanahalisi online Marehemu EDSON KAMUKARA leo mwili
wake umeagwa Jijini Dar es saalaam na kusafirishwa kwenda kupumzishwa
nyumbani kwao Bukoba baada ya kufariki ghafla Juzi Nyumbani kwake Mabibo
Jijini Dar es salaam.
EDSON KAMUKARA alifariki Dunia Terehe 25 mwezi huu nyumbani kwake kwa kile kinachotajwa kuwa ni ajali ya moto huku wengine wakisema ni ugonjwa wa malaria.
Habari za kifo chake zilianza kuenea kwa kasi majira ya saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo ambapo Taarifa hizo zilikuwa zikieleza kuwa ndugu EDSONI KAMUKARA alifariki baada ya kulipukiwa na jiko la GESI lililokuwa ndani kwake huku Taarifa nyingine kinzani ambazo zinazidi kuenezwa zikidai kuwa ugonjwa wa malaria ndio uliosababisha kifo chake.
Katika shuguli hiyo ya kuaga mwili huo katika viwanja vya LEADERS ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maswala ya habari wakiwemo mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Tanzania REGNALD MENGI,mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE,pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali na mashirika mbalimbali pamoja na wanahabari ambao ndugu EDSON alikuwa akishirikiana nao kwa ukaribu.
Nimekuwekea picha mbalimbali za matukio katika shughuli hiyo huku tukizidi kufuatilia kwa ukaribu sababu za kifo hiki cha ghafla

NISHATI YETU:-Tazama Picha 2 za Mtambo wa umeme vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa Kata ya Kabanga,wilayani Ngara mkoani Kagera.
Jumanne, 23 Juni 2015
Mwenyekiti Wa Jukwaa La Habari Tanzania Afunguka Mazito Kuhusu Mgombea Mmoja Wa Urais Kutaka Kumuua Soma Hapa Live!!!
Mhariri Mkuu wa Kampuni ya New Habari, ambao ni wachapishaji wa magazeti
ya Mtanzania, Bingwa na Dimba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF) ndugu, Absalom Kibanda, amemtupia kombora
mgombea Urais wa CCM. Kumbuka Kampuni ya New Habari, Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya New Habari (2006) ni Hussein Bashe ambaye ni Msemaji wa
Mgombea urais wa JMT Edward Lowassa.
Hapa nashindwa kuelewa Mhusika ni nani. Sababu siwezi kusema ni Membe sababu Membe alishatoa tamko kukana Kumdhuru Kipanda. Pitia hii thread Membe atoa tamko juu ya kutekwa kwa Kibanda na Waziri Membe akanusha kuhusika tukio la kumdhuru Mhariri Kibanda.
Kumbuka Bashe hawaivi chungu kimoja na Nape Nnauye. Na Nape Nnauye kaachiwa Jimbo la Mtama na Benard Membe. rejea hii Thread Bashe ajibu mashambulizi ya Nape Nnauye.

Mke Wa Mtu Sumu! Mwenye Mke Achomwa Kisu Na Mgoni Jijini Dar!!!
Riego
Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu akiuguza maumivu baada ya
kuchomwa kisu na mgoni wake. Tukio hilo la kinyume na kawaida ya
wanaofumania kufanya uhalifu, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita,
Mbezi ya Tangi Bovu.
Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu, Dar es Salaam anadaiwa
kuchomwa kisu kwenye koromeo katika jaribio la kuchinjwa na mgoni wake
aliyejulikana kwa jina moja la Jacob akiwa katika harakati za kumzengea
mkewe.
Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zinadai kwamba, Solo alivamiwa na mgoni wake huyo hatua chache toka nyumbani kwake ambapo wananchi walimsaidia baada ya kupiga kelele na walipofika eneo la tukio walimkuta akitokwa na damu huku akihangaika chini.

Mastaa Wa Bongo Wakiwa Na Watoto Wao
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)