Social Icons

Jumanne, 23 Juni 2015

Mke Wa Mtu Sumu! Mwenye Mke Achomwa Kisu Na Mgoni Jijini Dar!!!


Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu akiuguza maumivu baada ya kuchomwa kisu na mgoni wake. Tukio hilo la kinyume na kawaida ya wanaofumania kufanya uhalifu, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbezi ya Tangi Bovu.
Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu, Dar es Salaam anadaiwa kuchomwa kisu kwenye koromeo katika jaribio la kuchinjwa na mgoni wake aliyejulikana kwa jina moja la Jacob akiwa katika harakati za kumzengea mkewe.

Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zinadai kwamba, Solo alivamiwa na mgoni wake huyo hatua chache toka nyumbani kwake ambapo wananchi walimsaidia baada ya kupiga kelele na walipofika eneo la tukio walimkuta akitokwa na damu huku akihangaika chini.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni