Social Icons

Jumamosi, 27 Juni 2015

Huzuni Yatanda Dar,Mbowe,DK Slaa Waungana Na Wanahabari Kuaga Mwili Wa Edson Kamukara.

  Pichani ni mkurugenzi wa magazeti ya halisi piblisher na mwandishi nguli wa habari za uchunguzi tanzania SAID KUBENEA akiuaga mwili wa mfanyakazi mwenzake EDSON KAMUKARA LEO Jijini Dar es salaam Aliyekuwa mwandishi wa habari wa magazeti ya hali halisi publisher wazalishaji wa gazeti la mawio na mwanahalisi online Marehemu EDSON KAMUKARA leo mwili wake umeagwa Jijini Dar es saalaam na kusafirishwa kwenda kupumzishwa nyumbani kwao Bukoba baada ya kufariki ghafla Juzi Nyumbani kwake Mabibo Jijini Dar es salaam.
EDSON KAMUKARA alifariki Dunia Terehe 25 mwezi huu nyumbani kwake kwa kile kinachotajwa kuwa ni ajali ya moto huku wengine wakisema ni ugonjwa wa malaria.
Habari za kifo chake zilianza kuenea kwa kasi majira ya saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo ambapo Taarifa hizo zilikuwa zikieleza kuwa ndugu EDSONI KAMUKARA alifariki baada ya kulipukiwa na jiko la GESI lililokuwa ndani kwake huku Taarifa nyingine kinzani ambazo zinazidi kuenezwa zikidai kuwa ugonjwa wa malaria ndio uliosababisha kifo chake.
Katika shuguli hiyo ya kuaga mwili huo katika viwanja vya LEADERS ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maswala ya habari wakiwemo mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Tanzania REGNALD MENGI,mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE,pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali na mashirika mbalimbali pamoja na wanahabari ambao ndugu EDSON  alikuwa akishirikiana nao kwa ukaribu.
Nimekuwekea picha mbalimbali za matukio katika shughuli hiyo huku tukizidi kufuatilia kwa ukaribu sababu za kifo hiki cha ghafla







































































NISHATI YETU:-Tazama Picha 2 za Mtambo wa umeme vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa Kata ya Kabanga,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Pichani ni Mtambo wa UMEME Vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera.
Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga.

Jumanne, 23 Juni 2015

Mwenyekiti Wa Jukwaa La Habari Tanzania Afunguka Mazito Kuhusu Mgombea Mmoja Wa Urais Kutaka Kumuua Soma Hapa Live!!!

Mhariri Mkuu wa Kampuni ya New Habari, ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa na Dimba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ndugu, Absalom Kibanda, amemtupia kombora mgombea Urais wa CCM. Kumbuka Kampuni ya New Habari, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) ni Hussein Bashe ambaye ni Msemaji wa Mgombea urais wa JMT Edward Lowassa.

Hapa nashindwa kuelewa Mhusika ni nani. Sababu siwezi kusema ni Membe sababu Membe alishatoa tamko kukana Kumdhuru Kipanda. Pitia hii thread Membe atoa tamko juu ya kutekwa kwa Kibanda na Waziri Membe akanusha kuhusika tukio la kumdhuru Mhariri Kibanda.

Kumbuka Bashe hawaivi chungu kimoja na Nape Nnauye. Na Nape Nnauye kaachiwa Jimbo la Mtama na Benard Membe. rejea hii Thread Bashe ajibu mashambulizi ya Nape Nnauye.

Mke Wa Mtu Sumu! Mwenye Mke Achomwa Kisu Na Mgoni Jijini Dar!!!


Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu akiuguza maumivu baada ya kuchomwa kisu na mgoni wake. Tukio hilo la kinyume na kawaida ya wanaofumania kufanya uhalifu, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbezi ya Tangi Bovu.
Riego Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu, Dar es Salaam anadaiwa kuchomwa kisu kwenye koromeo katika jaribio la kuchinjwa na mgoni wake aliyejulikana kwa jina moja la Jacob akiwa katika harakati za kumzengea mkewe.

Taarifa zilizopatikana katika eneo la tukio zinadai kwamba, Solo alivamiwa na mgoni wake huyo hatua chache toka nyumbani kwake ambapo wananchi walimsaidia baada ya kupiga kelele na walipofika eneo la tukio walimkuta akitokwa na damu huku akihangaika chini.
 

Mastaa Wa Bongo Wakiwa Na Watoto Wao

WASANII WA BONGO FLEVA WAKIWA NA WATOTO WAO;THIS ARE THE BONGO FLAVA SUPERSTAR'S BUT THE GOOD NEWS IS .......THEY ARE FATHER TOO!! LOOK PHOTO'S HOW THEY ARE SHARING LOVES IN FATHER'S DAY!

Jumapili, 21 Juni 2015

Lowassa Adai Yeye Ndiye Atakayeleta Mabadiliko Ndani Ya CCM


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alisema kuwa muda wa mabadiliko aliyotabiri Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ni sasa na kwamba yeye ndiye anayeweza kuyaongoza.

Wakati Lowassa akisema hayo mjini Iringa, kada mwingine anayewania urais kwa kupitia chama hicho, William Ngeleja alikuwa mkoani Mwanza ambako alisema kuwa ana dhamira ya dhati na nia ya kuleta mabadiliko kwa maisha ya Watanzania.

Mjini Iringa, Lowassa alisema kuwa kwa sasa CCM inahitaji mabadiliko makubwa na akanukuu kauli ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 alipozungumzia haja ya chama hicho kujisahihisha.

“Baba wa Taifa alisema kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM,” alisema mbunge huyo wa Monduli kwenye hafla hiyo iliyofanyika Uwanja wa Samora mjini Iringa.

“Huu ni wakati wa mabadiliko. CCM ikijipanga inaweza kuleta mabadiliko na mtu wa kuleta mabadiliko hayo ni mimi,” alisema.

Lowassa alisema aliamua kuingia kwenye mbio za urais kwa sababu tatu, ambazo ni kufanya mabadiliko ndani ya CCM, kufanyia kazi tatizo la umaskini na kushughulikia tatizo la ajira kwa vijana.

Tudu Lissu Aibua Mazito Kuhusu Vyeo Vya Polisi.

 

Hakimu Denis Mpelembwa amepandishwa cheo kuwa 

hakimu mkazi na kuhamishiwa mkoani Kagera, siku 

moja tu baada ya kumuhukumu mbunge wa hai na 

mwenyekiti wa chadema taifa 

Freeman Mbowe kwenda jera mwaka 1 au faini milioni 1
Aliyekuwa RPC wa iringa kumuhanda alipandishwa cheo wiki 2 baada ya kumuuwa mwandishi wa habari daudi mwangosi.
Hakimu aliyemfunga mdude nyagali kwenda jera miaka mitatu au faini laki 2 naye alipandishwa cheo wiki 1 baada ya hukumu hiyo.
OCD aliyesababisha mauwaji arusha kwenye mkutano wa chadema alipandishwa cheo sasa ni RPC.
Akari wa jeshi la police bwana said aliyempiga risasi muuza magazeti pale morogoro wakati wa mkutano wa chadema alipewa cheo cha ukoplo.
askari waliowapiga risasi za matako na kuwauwa wachimbaji wadogowadogo wa madini kwenye mgodi wa buzwagi wamepandishwa vyeo ni masanjent na wengine ni makoplo na ma-OCD'
majaji na mahakimu wanang'ang'aniana kesi za chadema wahukumu ili wapandishwe vyeo,huku askari police nao wanajitahidi kupambikiza kesi kwa viongozi na wafuasi wa UKAWA ili wapande vyeo.