Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashirika wamelaani jaribio la mapinduzi yaliyotaka kufanyika nchini Burundi huku wakitaka utawala wa sheria kwa kuheshimu katiba na makubaliano ya arusha pamoja na kusogezwa mbele.
Mkutano huo umekubaliana kwa pamoja uchaguzi wa burundi usogezwe mbele hadi hali ya siasa itakapotengemaa.
Tofauti na matarajio ya wengi Rais Pierre Nkurunziza hakuweza kuhudhuria mkutano huo licha yakuwepo taarifa kuwa aliwasili jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo mkutano huo hakuweza kufanyika katika utaratibu ambao umepangwa kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kuwepo Mapinduzi nchini Burundi ambapo taarifa hizo zimeibua taharuki na wasiwasi miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wakiwemo viongozi kutoka nchi wanachama.
Katibu mkuu
wa umoja wa Mataifa Ban ki-Moon pichani amewataka wahusika wakuu nchini Burundi kuweka
uhasama baina yao kando ilikulinda taifa.
Rais wa
Burundi.
Kiongozi wa ''Mapinduzi'' Meja Jenerali Godefroid Niyombare.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni