Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa jana alisema kuwa muda wa mabadiliko aliyotabiri Baba wa
Taifa, Mwalimu Nyerere ni sasa na kwamba yeye ndiye anayeweza
kuyaongoza.
Wakati Lowassa akisema
hayo mjini Iringa, kada mwingine anayewania urais kwa kupitia chama
hicho, William Ngeleja alikuwa mkoani Mwanza ambako alisema kuwa ana
dhamira ya dhati na nia ya kuleta mabadiliko kwa maisha ya Watanzania.
Mjini Iringa, Lowassa
alisema kuwa kwa sasa CCM inahitaji mabadiliko makubwa na akanukuu kauli
ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 alipozungumzia haja ya chama
hicho kujisahihisha.
“Baba wa Taifa alisema
kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM
watayatafuta nje ya CCM,” alisema mbunge huyo wa Monduli kwenye hafla
hiyo iliyofanyika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
“Huu ni wakati wa mabadiliko. CCM ikijipanga inaweza kuleta mabadiliko na mtu wa kuleta mabadiliko hayo ni mimi,” alisema.
Lowassa alisema aliamua
kuingia kwenye mbio za urais kwa sababu tatu, ambazo ni kufanya
mabadiliko ndani ya CCM, kufanyia kazi tatizo la umaskini na
kushughulikia tatizo la ajira kwa vijana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni