Muonekano wa ghala hilo lilivyoathiriwa na mto huo.
Baadhi ya bidhaa
mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeteketea kwa
moto usiku wa kuamkia leo, katika ghala la kuhifadhia bidhaa za kampuni
ya Kahama oil mills wilayani kahama.
Akizungumza na wandishi
wa Habari ofisini kwake meneja mkuu wa kampuni hiyo William Matonange,
amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni kuripuka kwa baadhi ya
bidhaaa zenye asili ya kuripuka zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala
hilo.
Aidha meneja huyo
amesema kuwa bidhaa zilizoteketea zilikuwa na thamani ya zaidi ya
shilling billion 3 huku jengo likiwa lenye thamani zaidi ya shilling
billioni 1.
Akifafanua zaidi amesema
moto huo unasadikiwa ulianza usiku wa manane ambapo uligundulika majira
ya saa tisa usiku ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la polisi kitengo
cha zimamoto ambao walifika na kuanza kuuzima ambao ulidumu kwa masaa
sita.
Hata hivyo Matonange
amelipongeza jeshi la polisi mkoani shinyanga kwa juhuzi za kuimalisha
ulinzi katika zoezi la kuzima moto kutokana na wananchi walikuwa na
lengo la kuvamnia kiwanda hicho kwa ajili ya kwenda kupora mali wakati
jeshi la zimamoto likiendelea na zoezi la kuuzima moto huo.
Kwaupande wake kamanda
wajeshi la polisi mkoani shinyanga Justus Kamugisha amedhibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa uchunguzi unaendelea hivyo
taarifa zaidi zitatolewa baada ya wataalam kutoka kitengo cha bima
kufanya uchunguzi wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni