Charles Boniface Mkwasa 'Master' (Pichani) atashika timu kwa muda wakati TFF inasaka kocha wa kudumu wa Taifa Stars.
Kamati ya
utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfukuza kazi kocha
mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Mart Nooij pamoja na benchi zima la ufundi
la Taifa Stars baada ya kipigo cha goli
3 - 0 kutoka kwa Uganda kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya
Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN 2016) mchezo uliopigwa
kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar jana June 20, 2015 usiku.
Habari zinasema, Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa atashika timu kwa muda, akisaidiwa na Suleiman Matola wa Simba SC.
Kamati ya
Utendaji ya TFF ililazimika kufanya kikao cha dharula na “Katika kikao cha leo
pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa
ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya
tathmini ya mwenendo wa timu,”imesema taarifa ya TFF usiku huu.
“Kamati ya
utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo: -
1.Ajira ya
Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia tarehe 21/June/2015.
2. Benchi
lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.
3.Uongozi wa
TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa,”imemalizia
taarifa hiyo fupi iluyitolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya TFF,
Baraka Kizuguto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni