Social Icons

Ijumaa, 24 Aprili 2015

Ona Hapa Hii Official Video HD | Udsm Band - Limpopo Ni Sheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeda!!.


 https://www.youtube.com/watch?v=zrlC-BViZxwhttps://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=zrlC-BViZxw.

MWILI WA MWANAFUNZI KITETO ALIYEFARIKI KWA KUCHAPWA VIBOKO NA WALIMU WAFIKISHWA DODOMA

 

MWILI wa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui iliyoko Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, aliyedaiwa kufariki baada ya kuchapwa viboko na walimu wake, Emmanuel Mbigima (15), umefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Wakati mwili huo unafikishwa hospitalini hapo jana asubuhi, ulikuwa umewekwa kwenye gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ukisindikizwa na baadhi ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

"Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili.

“Tumechukua uamuzi wa kumleta hapa kwa sababu madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, walishindwa kubaini kichwa kimeathirika kwa kiasi gani kwa kuwa hawana vifaa vya uchunguzi vya kichwa.

“Hata hivyo, majibu ya uchunguzi wa awali yaliyotolewa katika hospitali hiyo, yalionyesha jicho la kulia lilivuja damu kwa ndani na pia mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko miguuni,” alisema Ngowi.

Naye mjomba wa marehemu, Michael Ezekiel alisema matukio ya wanafunzi kupigwa na kupoteza maisha yamekuwa yakijirudia shuleni hapo kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa.

“Mwaka jana kuna mtoto alipigwa na mwalimu akafariki, lakini mtuhumiwa alipelekwa mahakamani na baadaye kuachiwa kwa madai kuwa mtoto alikuwa ni mgonjwa,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Zainabu Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mwili huo na kusema uchunguzi bado unaendelea.

Awali, akizungumza na MPEKUZI baada ya mwanafunzi huyo kufariki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, aliwataja walimu waliohusika katika tukio hilo na ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, kuwa ni Machael Bajutta (28), Chalamilla Gereza (33) na Mwalimu Joyce Msiba (36).

Je,huyu ndio mwanamke mrembo duniani?


 

 Huenda asijihisi kuwa mrembo ,lakini Sandra Bullock ndiye mwanamke mrembo duniani.

Iwapo anaamini hilo au la ,nyota huyo wa filamu mwenye umri wa miaka 50 ametangazwa na gazeti la People magazine kama chaguo lake la kila mwaka la mwanamke mrembo duniani mwaka 2015.
Msanii huyo alidokezewa kuhusu habari hiyo kabla ya tangazo hilo kutolewa na jarida hilo.
Je tunakuuliza unakubaliana na uamuzi wa gazeti hilo kwamba Sandra Bullock ndiye mwanamke mrembo duniani?

VIDEO YA ‘NUSU NUSU’ YA JOH MAKINI IMEANZIA KWENYE TV KUBWA DUNIANI YA MTV.. STORI IKO HAPA

 

Kingine ambacho nimekishuhudia muda mfupi uliopita kwenye Channel ya MTV #322 on DSTV ni hii video ya Mbongo mwingine.. Mkali wa Hiphop toka kundi la WEUSI, Joh Makini ikitambulishwa rasmi kwa mara ya kwanza. Wimbo unaitwa Nusu Nusu, Joh kamshirikisha mweusi mwingine mkali wa Chorus, G Nako. Ni furaha kumuona mwana Hiphop kwenye Headlines za TV kubwa...

Hii ndio Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kuhusu Tukio la Majambazi kuua na Kupora Fedha April 20,2015.







Majambazi yaliyokuwa na silaha yalivamia gari mali ya Kampuni ya Bonite na kuwamiminia risasi dereva wa gari hilo  na mlinzi wa Kampuni hiyo  kisha kupora fedha na kutokomea kusikojulikana.

 Taarifa zinadai kuwa dereva na mlinzi wa gari lililoshambuliwa walifariki palepale kutokana na kupigwa risasi nyingi sehemu mbalimbali za miili yao.Tukio hilo limetokea April 20, 2015 mjini Moshi ambapo majambazi wanne waliokuwa kwenye pikipiki walivamia gari la Bonite lililokuwa likitoka kuchukua pesa za mauzo ya kampuni hiyo.

Alhamisi, 23 Aprili 2015

Kwa mara ya kwanza, Jux athibitisha kuwa Vanessa Mdee ni mpenzi wake!! Msikie Hapa!!

 

 

 

VPL 2014/2015:-Ijumaa April 23, 2015 Yanga SC v Ruvu Shooting huku mechi mbili tu Kuwapa Ubingwa wa Msimu huu.


MSIMAMO VPL 2014/2015.
Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC, hapo kesho Ijumaa April 24, 2015 wanaingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting wakijua ushindi wa Mechi hiyo na mwingine hapo Jumatatu dhidi ya Polisi Moro utawapa Ubingwa  msimu huu huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.

Hivi sasa Yanga SC wako kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22 wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 22 na Simba SC wapo Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 23.
Hivyo Yanga SC , ambao tayari wameshakuwa moja ya Timu mbili zitakazocheza Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika Msimu ujao, wanahitaji Pointi 6 tu kuwa bila Bingwa bila kujali nini mpinzani wake Azam FC anakifanya.
Azam FC Jumamosi April 25, 2015 wanacheza Nyumbani kwao na Stand United na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu kitu ambacho pia kitawasaidia kukwepa Simba, ambao Jumatano waliitwanga Mgambo JKT 4-0, kuwapiku Nafasi ya Pili.
LIGI KUU VODACOM 2014/2015 RATIBA.