UHALIFU:-
Majambazi
yaliyokuwa na silaha yalivamia gari mali ya Kampuni ya Bonite na kuwamiminia
risasi dereva wa gari hilo na mlinzi wa
Kampuni hiyo kisha kupora fedha na kutokomea
kusikojulikana.
Taarifa
zinadai kuwa dereva na mlinzi wa gari lililoshambuliwa walifariki palepale
kutokana na kupigwa risasi nyingi sehemu mbalimbali za miili yao.Tukio hilo
limetokea April 20, 2015 mjini Moshi ambapo majambazi wanne waliokuwa kwenye
pikipiki walivamia gari la Bonite lililokuwa likitoka kuchukua pesa za mauzo ya
kampuni hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni