Social Icons

Alhamisi, 23 Aprili 2015

VPL 2014/2015:-Ijumaa April 23, 2015 Yanga SC v Ruvu Shooting huku mechi mbili tu Kuwapa Ubingwa wa Msimu huu.


MSIMAMO VPL 2014/2015.
Vinara wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC, hapo kesho Ijumaa April 24, 2015 wanaingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting wakijua ushindi wa Mechi hiyo na mwingine hapo Jumatatu dhidi ya Polisi Moro utawapa Ubingwa  msimu huu huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.

Hivi sasa Yanga SC wako kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 22 wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Azam FC wenye Pointi 42 kwa Mechi 22 na Simba SC wapo Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 23.
Hivyo Yanga SC , ambao tayari wameshakuwa moja ya Timu mbili zitakazocheza Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika Msimu ujao, wanahitaji Pointi 6 tu kuwa bila Bingwa bila kujali nini mpinzani wake Azam FC anakifanya.
Azam FC Jumamosi April 25, 2015 wanacheza Nyumbani kwao na Stand United na ili kuweka uhai matumaini yao finyu ya kutetea Taji watalazimika kushinda tu kitu ambacho pia kitawasaidia kukwepa Simba, ambao Jumatano waliitwanga Mgambo JKT 4-0, kuwapiku Nafasi ya Pili.
LIGI KUU VODACOM 2014/2015 RATIBA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni