Social Icons

Jumatatu, 27 Aprili 2015

MATUKIO MUHIMU:-Taswira Picha ya Utoaji wa Nishani za Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano April 26,2015.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Bw.Damian Zefrini Lubuva baada ya kumvalisha  Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana April 26,2015 viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha nishani Bw.Aboud Talib Aboud wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Tatu katika  viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa jamhuri ya Muungano Dk.Mohammed gharib Bilali pamoja na Viongozi wengine wakiwa  katika picha ya pamoja baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Cpl Laura Philip Mushi  Nishani ya Ushupavu wakati wa utoaji wa Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Madaraja mbali mbali katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Tanzania wakisimama wakati wimbo wa taifa ukipigwa baada ya kumalizika hafla ya sherehe ya utoaji wa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili,Tatu na Nne jana katika viwanja vya Ikulu Jijini Dares SalaamMiongoni mwa Wananchi na Viongozi walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao,[Picha na Ikulu,] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) na makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe za utoaji wa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali  katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam janaMiongoni mwa Viongozi na Wananchi  walioteuliwa kutunikiwa nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano wa madaraja mbali mbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kutunikiwa nishani zao ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jana,[Picha na Ikulu,] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimvalisha  Bw.Mabrouk Jabu Makame Nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano Daraja la Pili katika hafla iliyofanyika jana viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam

Msimamo wa Rais wa Burundi ni upi?

Baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake kugombea urais kwa muhula wa tatu.Maandamano makubwa yameendelea nchini humo na kugharimu maisha ya watu ,waandamaji hao wanadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi waliokuwa wakijaribu kuyadhibiti maandamano hayo.wafuasi hao wameapa kuendelea na maandamano hayo, hadi rais Nkurunzinza atakapobadili uamuzi wake wa kuwania urais kwa muhula mwingine.


Mwandishi wetu Regina Mziwanda ,amefuatilia kinachoendelea Burundi kwa sasa na amezungumza na Msemaji wa Rais wa Burundi Jervier Abayeho na kwanza amemuuliza msemaji huyo kuwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anafikiria kufanya mazungumzo na upinzani ili kuondoa mvutano unaoendelea sasa nchini humo?
 

TANGAZO


OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM - TAMISEMI)
AJIRA MPYA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA NA WALIMU KWA SHULE
ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2014/15
A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
Ofisi ya Waziri Mkuu  - TAMISEMI inatangaza  ajira ya wahitimu wa mafunzo ya
ualimu  na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa  kama
ifuatavyo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi  11,366;
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa  masomo
ya  sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari
B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14
wamepangwa  pamoja na walimu wa sekondari  wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi
wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari,
cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
v. fedha za kujikimu kwa muda wa  siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari
(ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
                                                                        Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA.

Ajira Mpya za Walimu Kwa Mwaka 2015.

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa.


Kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma taarifa zifuatazo:




 

SERIKALI YAZIFUTIA USAJILI TAASISI (NGOs) 24 ZISIZO ZA KISERIKALI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa asasi za kiraia (NGOs) zilizoorodheshwa hapa chini zimefutiwa usajili wake kuanzia tarehe ya tangazo hili; kutokana na kukiuka matakwa ya kisheria katika utendaji kazi.

Kwa tangazo hili, uhalali wa kufanya kazi kwa mashirika haya umekoma na kuendelea kufanya kazi baada ya kufutiwa usajili ni kosa la jinai. Viongozi wa NGOs tajwa wanaagizwa kurejesha vyeti vya usajili kwa Msajili ndani ya siku thelathini baada ya tangazo hili.

Orodha hii inahusisha mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Tanzania. Orodha ya mashirika ya ndani inachambuliwa na itatangazwa muda wowote kuanzia sasa;

1. AFRICA CALL MANAGEMENT INSTITUTE (ACMI)

2. AFRICA CENTRE FOR PEACE AND DEVELOPMENT

3.AIDOS - TANZANIA
4. ASSOCIAZIONE CASAGLIA ROSETTA
5. COPE-COOPERATION DEVELOPMENT COUNTRIES
6. DAN CHURCH AID
7. DIGITAL LINKS TANZANIA
8. EKKLESIA INTERNATIONAL TANZANIA
9. FEED THE CHILDREN TANZANIA

10. GLOBAL ALLIANCE FOR AFRICA TANZANIA
11. GLOBAL VESSELS TANZANIA

12. HEALTH DEVELOPMENT INTERNATIONAL (HDI)

13. EMPOWERMENT RESULT IN BALANCE AND EQUALITY (ERBAAQ)
14. MENNONITE CENTRAL COMMITTEE IN TANZANIA (MCCTZ)

15. MIDMAY INTERNATIONAL

16. PAMOJA INC.

17. PAN AFRICAN WHEEL CHAIR BUILDERS ASSOCIATION (PAWBA)

18. JAMII ONLUS

19. THE BALM IN GILEAD TANZANIA

20. THE INTERNATIONAL INSTITUTE OF THE IOGT - NTO MOVEMENT

21. TROCAIRE

22. VETERINARIANS WITHOUT BORDERS GERMANY(VSF- GERMANY)

23. WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY

24. WORLD SOCIETY FOR THE PROTECTION OF ANIMALS (WSPA),

Imetolewa na;
OFISI YA MSAJILI
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

 

JE KWA HALI KAMA HII BURUNDI INAELEKEA WAPI?

Uamuzi wa chama tawala nchini Burundi wa kumteua Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena urais tarehe 26 mwezi Juni unaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi
 Ni ishara inayohatarisha demokrasia barani Afrika. Kulikoni katika nchi za maziwa makuu? Viongozi wanazidi kungang'ania mamlaka hawataki kuyaachia na wanazidi kufarakana na watu wao na wanajiweka mbali na kile wanachokitaka wananchi wao.Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameibadilisha katiba ya nchi yake ili kumwezesha kutawala daima. Alipoapishwa mnamo mwaka wa 1986 Museveni alisema kuwa tatizo la bara la Afrika ni kwamba viongozi wake wanakaa madarakani kwa muda mrefu na hivyo kuyaweka mazingira ya kuweza kutenda uhalifu bila ya kuwajibishwa, kujenga ufisadi na mfumo wa uchumi wa kuwapendelea ndugu na marafiki.

Pia nchini Rwanda na katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ,Marais Paul Kagame na Joseph Kabila wanatoa ishara kuonyesha kana kwamba bila ya wao mambo hayawezi kusonga mbele katika nchi zao.Nchini Burundi chama tawala mwishoni mwa wiki kilimteua Rais Pierre Nkurunziza kuwa mgombea wake katika uchaguzi wa rais na hivyo kuwania muhula wa tatu. Wapinzani walianza kuupinga uamuzi huo siku nyingi kwani ulionekana unakuja.Katiba ya Burundi hairuhusu muhula wa tatu. Lakini serikali inatoa hoja ya paukwa pakawa kwamba muhula wa kwanza ambao Rais Nkurunziza aliutumikia huwezi kutiwa katika hesabu, ati kwa sababu wakati huo hakuchaguliwa na umma bali na Bunge.
 Maalfu wakimbilia nchi jirani
Maalfu kwa maalfu ya wananchi wa Burundi wameshaikimbia nchi yao na kwenda katika nchi za jirani kutokana na hofu. Na maalfu kwa maalfu walijitokeza barabarani mwishoni mwa wiki kufanya maandamano mengine. Idara za usalama zilitumia ukatili: waandamanji na polisi walipambana na waandamanaji wasiopungua wawili waliuliwa kwa kupigwa risasi na polisi. Amani nchini Burundi ambayo bado ni teketeke imo hatarini. Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka wa 1993 hadi 2005, watu 300,000 walikufa nchini humo. Hatari ya mvutano uliopo sasa ya kuitumbukiza Burundi katika vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe ni kubwa.Hatari nyingine inatokana na tawi la vijana waliopo karibu sana na serikali-Imbonerakure. Vijana hao wanawatishia wananchi wazi wazi, na hatari kubwa zaidi ni kwamba wanazo silaha.
Upande wa upinzani uliususia uchaguzi wa mwaka 2005 kwa sababu kwa mtazamo wa wapinzani hao hapakuwapo msingi wa kuwezesha kufanyika uchaguzi huru na wa haki. Rais na chama chake cha CNDD-FDD wametawala kidikteta nchini Burundi katika miaka iliyopita. Wapinzani wanazibwa midomo na vyombo vya habari vinatishwa. Mashirika ya haki za binadamu kama vile Human Rights Watch yameripoti juu ya mauaji ya kiholela, mauaji yanayofanywa kwa sababu za kisiasa na pia yamearifu juu ya wapinzani kukamatwa ovyo. Hayo lazima yakomeshwe.Lakini kwa bahati mbaya miito iliyotolewa na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kwa jumla haijasaidia kitu. Sasa inabidi nchi jirani ziingilie kati, lakini ni nani anaeweza kurusha jiwe la kwanza, kwani ukimwondoa Rais Jakaya Kikwete, viongozi wengine wote wanataka kuendelea kungang'ania mamlaka.
Licha ya kuwa nchi ndogo na masikini kabisa duniani, Burundi pia imo katika ajenda ya kisiasa ya jumuiya ya kimataifa. Miito peke yake haitasaidia kitu.
Hatua thabiti lazima zichukuliwe,na kwa haraka, ili mgogoro wa nchini Burundi usiendelee kutokota na kuitumbukiza nchi hiyo katika vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe. La sivyo hapatakuwa na matumaini mema juu ya uchaguzi wa bunge mnamo mwezi wa Mei, uchaguzi wa rais mnamo mwezi wa Juni na kwa mustakabal wa Burundi kwa jumla .
Na hasa katika mwaka huu wa adhimu kwa Afrika ,ambapo bara hilo lilianza kuelekea katika njia nzuri, baada kufanyika uchaguzi ulioleta mabadiliko ya uongozi kwa amani, nchini Nigeria, kinachotokea Burundi ,ni jambo linalosababisha wasi wasi mkubwa.

Chanzo: DW.

Jumapili, 26 Aprili 2015

Matukio Picha Maadhimisho Miaka 51 ya Muungano Tanganyika na Zanzibar April 26/2015

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMRRais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMRRais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMRRais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMRRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMRRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMRRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMRRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMR

Dj fran k'ee chilling-jingle

HATIMAYE WASHINDI WA SHINDANO LA SHIKA NDINGA LA 93.7 EFM WAPATIKANA BAADA YA MCHUANO MKALI

Hatimaye Washindi washindano la shika ndinga la 93.7 EFM wapatikana baada ya mchuano mkali

uliofanyika jana tarehe 25 mwezi wan ne katika viwanja vya Tanganyika pekas kawe. Fainali hiyo

ilihusisha washiriki kumi kutoka katika wilaya 3za mkoa wa dar-es-salaam kumi tano kati yao wakiwa wanawake na kumi na tano wakiwa ni wanaume.

Shindano hilo lilihudhuriwa na mkuu wa mkoa mheshimiwa Sadiq Mecky Said akiwa kama mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya kinondoni mheshimiwa Paul Makonda na naibu meya wa wilaya ya temeke mheshimiwa Jumma mkenga.


 DU7C4958(1)

Akiongea jana mheshimiwa Sadiq Said alisema ni ubunifu wa hali ya juu ulioneshwa na kituo cha 93.7 EFM kwa kuanzisha shindano la aina yake ambalo litaongeza ajira kwa vijana na

kuinua hali zao za uchumi ,pia aliwahasa washindi kutumia ndinga walizoshinda ili kujiendeleza kiuchumi.

Kwa upande wake mheshimiwa Paul Makonda alisema vijana wajifunze kujitokeza katika mashindano kama haya maana zaidi ya kuburudishayanabadilisha maisha yao kwa namna yatofauti.

Washindi waliojishindia ndinga kwa upande wa wanaume ni Gabriel Robert kutoka wilaya ya temeke mwenye umri wa miaka 36 na Stella Joseph kutoka wilaya ya ilala mwenye umri wa miaka 26 ambao kwa pamoja wamesema shindano halikuwa rahisi na wanafuraha kubwa ya

kujishindia gari hizo ambazo watazitumia katika biashara zao aidha wameishukuru redio ya

93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na kuwashauri wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali wasikilizaji wake.

 DU7C5113

 Gabriel Robert kutoka wilaya ya temeke


 DU7C5105

  Stella Joseph kutoka wilaya ya ilala



DU7C5011   DU7C5053
 DU7C5031DU7C5129.png

Jumamosi, 25 Aprili 2015

NAY WA MITEGO NA SHAMSA SASA NI MKE NA MUME,SHAMSA AKUTWA NYUMBANI KWA NAY ASUBIHI AKIWA NA KANGA MOJA

Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.

  Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.

Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.

Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.
 
 
...Wakipozi kimahaba.

“Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:

“Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”
  
...Wakipata msosi.
Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa mwigizaji huyo.

MOTO WATEKETEZA GHALA LA BIDHAA ZA KAMPUNI YA KAHAMA OIL MILLS YA MJINI KAHAMA

 

Muonekano wa ghala hilo lilivyoathiriwa na mto huo.

Baadhi ya bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, katika ghala la kuhifadhia bidhaa za kampuni ya Kahama oil mills wilayani kahama.

Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake meneja mkuu wa kampuni hiyo William Matonange, amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni kuripuka kwa baadhi ya bidhaaa zenye asili ya kuripuka zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala hilo.
 
Aidha meneja huyo amesema kuwa bidhaa zilizoteketea zilikuwa na thamani ya zaidi ya shilling billion 3 huku jengo likiwa lenye thamani zaidi ya shilling billioni 1. 

Akifafanua zaidi amesema moto huo unasadikiwa ulianza usiku wa manane ambapo uligundulika majira ya saa tisa usiku ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la polisi kitengo cha zimamoto ambao walifika na kuanza kuuzima ambao ulidumu kwa masaa sita.
 
Hata hivyo Matonange amelipongeza jeshi la polisi mkoani shinyanga kwa juhuzi za kuimalisha ulinzi katika zoezi la kuzima moto kutokana na wananchi walikuwa na lengo la kuvamnia kiwanda hicho kwa ajili ya kwenda kupora mali wakati jeshi la zimamoto likiendelea na zoezi la kuuzima moto huo.
Kwaupande wake kamanda wajeshi la polisi mkoani shinyanga Justus Kamugisha amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa uchunguzi unaendelea hivyo taarifa zaidi zitatolewa baada ya wataalam kutoka kitengo cha bima kufanya uchunguzi wao.
 

KAMA ULIKUWA HUJUI:NDANI YA MIAKA 10 IJAYO TEMBO TANZANIA WATATOWEKA.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika mkutano uliohusisha wadau wa mashirika ya Kimataifa na asasi za kijamii ukiwa na lengo la ushirikishaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.

Waziri Nyalandu akiendelea kutoa ufafanuzi.

 Waziri Nyalandu akikazia jambo.

 Naibu Waziri wa Maliaisli na Utalii, Mahmoud Mgimwa akitoa salamu kwa wadau wa taasisi za kirai. Kushoto Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.

 

Mratibu wa Uhakiki wa Ubora kutoka Haki Elimu, Robert Mihayo akitoa maoni kwa Waziri Mh. Nyalandu ambapo amemuomba kushirikisha wadau wa elimu katika kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ili kuwaanda vijana ambao ni taifa la kesho.


Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society, Francis Kiwanga akishiriki kutoa maoni katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori pamoja na kutokemeza ujangili wa Tembo.
 Mwandishi wa gazeti la Daily News, Diriham Kimathi akiuliza swali kwa Waziri Nyalandu (hayupo pichani).

Wadau kutoka asasi za kijamii na mashirika ya kimataifa waliohudhuria mkutano ulioitishwa na Waziri Nyalandu ambao umefanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


...wakisikiliza kwa makini.
 
 

  Waziri Nyalandu akisalimiana na baadhi ya wadau kutoka mashirika ya kimataifa na asasi za kijamii waliohudhuria mkutano huo.

 

 Mdau kutoka Tanzania Association on Climate Change, Ali Said Mosee akitoa maoni yake juu ya kuhusiana na nini kifanyike katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori katika mkutano uliotishwa na Waziri Nyalandu (hayupo pichani).

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kama watanzania wasiposhirikiana katika kudhibiti ujangili wa Tembo waliopo watatoweka kabisa katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye mkutano wa ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika wizarani kwake.

“Uhifadhi kama tunavyoujua, hautaweza kufanikiwa kama kila mtu kwenye nchi hii atafikiria ni kazi ya serikali kuu peke yake.

Na vilevile kama kila mtu atafikiria ni kazi ya wahifadhi peke yao”. alisema Nyalandu kwenye mkutano huo.

Nyalandu alibainisha kuwa, majadiliano hayo, yatakuwa chachu kubwa ya maendeleo katika wizara hiyo huku akiwashukuru wadau hao mbalimbali wakiwemo wanahabari kwa kufika kwao, ili kuangalia suala la uhifadhi kwa mapana yake.

Alisema wakati ujangili wa Tembo nchini umeshamiri sana, wakati umefika kwa watanzania kuhakikisha kwamba wanakomesha hali hiyo ili taifa kuendelea kuwa na wanyama wake.

Alisema mathalani Tembo katika hifadhi ya Selous wamepungua kutoka Tembo 38,975 katika sensa ya mwaka 2009 hadi Tembo 1,384 kwa sensa ya mwaka 2014 na akasema kwa kasi hiyo katika miaka 10 ijayo Tembo Tanzania wataisha kabisa.

“Hili ni muhimu watu wakafahamu, upana wa hivi vita ni mkubwa kiasi gani na watu wanaohusika ni wengi kiasi gani ndani na nje ya nchi," alisema Nyalandu akiongeza kuwa mitandao ya kihalifu imetanda ulimwenguni kote.

Alisema suala la hifadhi halipo kwa wanyama pekee bali lipo katika upana wote na hata katika misitu.

Alisema ili kukabiliana na ukatwaji hovyo wa miti kutoka katika misitu ya miombo wanajipanga kuhakikisha kwamba miombo inayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia inakamatwa ili kulinda miombo iliyopo magharibi ya nchi.

Akizungumzia suala la mifugo na mbuga zinazopakana nazo amesema kwamba wanaanda rasimu ya kuhakikisha kwamba kuna mahusiano mazuri kati ya wenye mifugo na hifadhi wakiwa tayari kuyaachia baadhi ya maeneo kwa lengo la kuhakikisha kwamba wafugaji hawaingizi mifugo yao katika hifadhi.

Aidha amesema kwamba wanajipanga namna ya kuhakikisha kwamba hakuna mgongano wa maeneo kati ya wanyama na binadamu na kwamba wanavijiji wanafundishwa namna ya kuishi na wanyama katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa.

Aidha alisema kwamba meno ya Tembo kilo 1,763 yalikamatwa mwaka jana na jitihada zinaendelea za kukabiliana na majangili kwa kutanua mtandao wa kiintelejensia ndani na nje.

Alisema kwa sasa wanamsaka raia wa China anayeshutumiwa kutorosha nyara za serikali kwa kushirikiana na jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol).

Kwa nje ya nchi, meno ya Tembo yaliyokamatwa, Kilo 40 katika miji ya Hong Kong, China.

Aidha alisema watuhumiwa 1,711, walikamatwa kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana na kesi zao zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini. Pia silaha 85 zimekamatwa ikiwemo silaha za kivita ambazo walikuwa wakizitumia mbugani.

Alisema ukichanganya na silaha zilizokamatwa kwenye operesheni tokomeza, jumla silaha 1,199 zimekamatwa.

Kwa upande wake, Ali Said Mosee aliyehudhuria mkutano huo kutoka Tanzania Association on Climate Change, alishauri ushirikishaji wa wadau mbalimbali kutatua migogoro kwenye mipaka ya mbuga na pia mgongano wa kimaslahi kati ya hifadhi na wanadamu.

Aidha wadau walishauri Wizara kuhakikisha inapunguza misafara ya wanyama ya kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwemo kwa kuzalisha miti na mazao yanayopendwa na wanyama hao.

“Wanyama wetu wanatakiwa wafanyiwe utafiti na kujua nini Nyati anapendelea kula porini, basi wapande hiyo miti na vyakula vyake kwa ujumla hata kwa Tembo hivyo hivyo.Wapande hiyo miti hapa hapa kwani hata siye binadamu tunavyovyakula tunavyovipenda, naamini hata kwa wanyama ni hivyo hivyo, rai yangu ni kuwa tufanye utafiti na kujua ili kuzuia misafara hii” alisema Ali Said Mosee.

Tanzania inahifadhi za taifa 16 na asilimia 40 ya ardhi ya nchi ni maeneo yaliyohifadhiwa. Kati ya maeneo hayo yaliyohifadhiwa hadi mwezi uliopita mwaka huu 2015, maeneo 19 yanamilikiwa na wananchi na yameshasajiliwa. Pia alisema kwamba kuna mapori ya akiba, 28 nchi nzima.

“Watu wengi wanadhani kwamba misitu yote inamilikiwa na serikali kuu. Ukweli ni kwamba serikali kuu inamiliki asilimia 35 tu ya misitu ya nchi yetu, misitu mingine yote inamilikiwa na vijiji, wilaya na watu binafsi asilimia 7. " alibainisha waziri huyo.

Aliwataka watendaji wa Serikali za mitaa kukabiliana na changamoto ya kutoweka kwa kasi kwa misitu ili taifa lisitumbukie katika jangwa.