HATIMAYE WASHINDI WA SHINDANO LA SHIKA NDINGA LA 93.7 EFM WAPATIKANA BAADA YA MCHUANO MKALI
Hatimaye Washindi washindano la shika ndinga la 93.7 EFM wapatikana baada ya mchuano mkali
uliofanyika jana tarehe 25 mwezi wan ne katika viwanja vya Tanganyika pekas kawe. Fainali hiyo
ilihusisha washiriki kumi kutoka katika wilaya 3za mkoa wa
dar-es-salaam kumi tano kati yao wakiwa wanawake na kumi na tano wakiwa
ni wanaume.
Shindano hilo lilihudhuriwa na mkuu wa mkoa mheshimiwa Sadiq Mecky
Said akiwa kama mgeni rasmi, mkuu wa wilaya ya kinondoni mheshimiwa Paul
Makonda na naibu meya wa wilaya ya temeke mheshimiwa Jumma mkenga.
Akiongea jana mheshimiwa Sadiq Said alisema ni ubunifu wa hali ya juu
ulioneshwa na kituo cha 93.7 EFM kwa kuanzisha shindano la aina yake
ambalo litaongeza ajira kwa vijana na
kuinua hali zao za uchumi ,pia aliwahasa washindi kutumia ndinga walizoshinda ili kujiendeleza kiuchumi.
Kwa upande wake mheshimiwa Paul Makonda alisema vijana wajifunze
kujitokeza katika mashindano kama haya maana zaidi ya
kuburudishayanabadilisha maisha yao kwa namna yatofauti.
Washindi waliojishindia ndinga kwa upande wa wanaume ni Gabriel
Robert kutoka wilaya ya temeke mwenye umri wa miaka 36 na Stella Joseph
kutoka wilaya ya ilala mwenye umri wa miaka 26 ambao kwa pamoja wamesema
shindano halikuwa rahisi na wanafuraha kubwa ya
kujishindia gari hizo ambazo watazitumia katika biashara zao aidha wameishukuru redio ya
93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na kuwashauri wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali wasikilizaji wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni