Mara baada ya kuelezwa
kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana
‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na
mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.
Baada ya kutonywa
‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya
Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga
moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi
alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba
wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana
zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake
kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay
nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo
na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku
wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.
...Wakipozi kimahaba.
“Kwani tatizo lipo wapi?
Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kama
unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua kupenda na
kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
“Yeah! Kwa sasa hakuna
project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi kuwazungumzia
wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa sasa, ninampenda
Shamsa.”
...Wakipata msosi.
Nay na Shamsa walianza
uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai kwamba alimnasa mpenzi
wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa sita hivyo kuamua
kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa mwigizaji huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni