EDSON KAMUKARA alifariki Dunia Terehe 25 mwezi huu nyumbani kwake kwa kile kinachotajwa kuwa ni ajali ya moto huku wengine wakisema ni ugonjwa wa malaria.
Habari za kifo chake zilianza kuenea kwa kasi majira ya saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo ambapo Taarifa hizo zilikuwa zikieleza kuwa ndugu EDSONI KAMUKARA alifariki baada ya kulipukiwa na jiko la GESI lililokuwa ndani kwake huku Taarifa nyingine kinzani ambazo zinazidi kuenezwa zikidai kuwa ugonjwa wa malaria ndio uliosababisha kifo chake.
Katika shuguli hiyo ya kuaga mwili huo katika viwanja vya LEADERS ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maswala ya habari wakiwemo mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Tanzania REGNALD MENGI,mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE,pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali na mashirika mbalimbali pamoja na wanahabari ambao ndugu EDSON alikuwa akishirikiana nao kwa ukaribu.
Nimekuwekea picha mbalimbali za matukio katika shughuli hiyo huku tukizidi kufuatilia kwa ukaribu sababu za kifo hiki cha ghafla





















