Wakati
watu kama Sitta wakikodi magari maalum kwa ajili ya zoezi la utafutaji
wadhamini na watu kama Makongoro wakijikongoja na magari ya marafiki
zao; hali imekuwa tofauti kabisa kwa Lowassa kwani yeye amepatiwa ndege
maalum kwa ajili ya shughuli hiyo ya kutafuta wadhamini!
Ndege hiyo 'private jet'
ambayo Lowassa amepatiwa na wafadhili wake katika safari yake hii ya
matumaini imetolewa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha Lowassa anazunguka
mikoa yote nchini bara na visiwani kabla ya julai 12 na 13 ili
akamilishe zoezi la kuwapata wadhamini 435 nchi nzima ili kufanikisha
sharti la chama kwa wagombea nafasi ya urais.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni