(1) Kangi Lugola (Mwibara CCM)
Mbunge huyo
machachari wa chama tawala aliibuka bungeni na staili ya aina yake wakati wa
kujadili hotuba ya bajeti. Aliingia ndani ya ukumbi wa Bunge akiwa na begi
lililojaa bidhaa za kawaida zilizoagizwa kutoka nje ambazo zinawezekana
kutengenezwa nchini, akisema uagizaji huo ndiyo unaoporomosha thamani ya
Shilingi ya Tanzania.
Lugola,
ambaye aliwahi kuingia bungeni na kofia ya kininja, ili afiche sura yake kwa
watu aliotaka kuwasema waziwazi, alikuwa akiilaumu Serikali kwa kushindwa
kuzuia bidhaa zinazotoka nje akisema fedha nyingi za kigeni zinatumika kwa
matumizi ambayo hayastahili.
“Nimekuja na
kontena zima, kama ingewezekana kuingia nalo hapa, ningeingia nalo humu ndani,”
alisema.
Bidhaa
alizoleta ni dodoki za plastiki kutoka China, soksi za Marekani, leso za China,
chaki (Kenya), pipi (Kenya), nyembe (China), pamba za masikio kutoka China,
vijiti vya kusafisha meno (China), bazoka (Kenya), viberiti (Kenya) pamoja na
rula na penseli kutoka China.
Alisema
haiwezekani kwa Tanzania yenye rasilimali nyingi ambazo zingeweza kutumika
kutengeneza bidhaa hizo, inatumia fedha za kigeni kuziagiza kutoka nje, “kisha
tunalalamika kuporomoka kwa shilingi”. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni