MTANGAZA NIA WA URAIS MALIKI MALUPU.
Hamasa
ya wanaCCM kutangaza nia ya kuwania urais imemwibua mwanafunzi Shahada
ya Uzamili ya Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Maliki
Malupu (34).
Malupu
alitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM akiahidi kushughulikia
suala la elimu, afya, kilimo na michezo huku akijua kuwa umri wake
haujatimia miaka 40 inayotakiwa kikatiba.
Akitangaza
nia hiyo mjini Morogoro jana, Malupu alisema kutokana na uaminifu na
uadilifu wake, ameamua kuwania nafasi hiyo pamoja na mambo mengine kwa
kuwa ni haki yake kikatiba.
Alipoulizwa
atatimizaje nia yake hiyo bila kuwa na sifa kikatiba, alisema vifungu
vya katiba vinavyotaja umri vina utata, hivyo ameamua kuingia
kuvitafutia suluhisho.
“Unajua
ibara ya 39 (1) (b) inasema lazima utimize miaka 40, lakini ibara (d)
inasema mtu mwenye sifa za kuwa mbunge au mjumbe wa baraza la
wawakilishi anaweza kuwania urais,” alisema akifafanua kuwa yeye ana
sifa hizo.
Akieleza
sababu nyingine zilizomsukuma kuwania urais, Malupu alisema kuwa ni
kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa kikamilifu kwa kuwa muda mrefu
imekuwa ikichezewa na baadhi ya viongozi.
Alisema
muundo wa sekta hiyo unapaswa kurekebishwa kwa ama kufutwa au
kuondoshwa utaratibu wa kupanga viwango vya ufaulu wa GPA kwa wanafunzi
wa elimu ya sekondari katika mitihani ya kidato cha sita na cha nne.
Alisema
utaratibu huo haufai kwa kuwa hautoi matokeo ya kuboresha maarifa kwa
wanafunzi, pia unawaathiri wanafunzi kisaikolojia katika kujitofautisha
wao na wanafunzi wa elimu ya juu.
“Nitahakikisha
naboresha mitalaa kwa masomo ya kidato cha nne na cha sita ili kuleta
weledi wa kina na wa kutosha, nitaboresha mazingira ya watumishi sekta
ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na stahiki za walimu wa
msingi hadi vyuo,” alisema.
Katika
mkutano wake wa saa 1.30, Malupu alisema atahakikisha anadhibiti suala
la maprofesa kuacha kazi yao ya weledi na kukimbilia katika siasa na
ataboresha stahiki zao na mishahara kwa kuwalipa vizuri wanaofundisha
vyuo vya Serikali na binafsi bila ubaguzi wowote ili kuimarisha sekta ya
elimu ngazi vyuo vikuu.
Malupu
alisema ataitazama sekta ya kilimo kwa kuongeza vyuo vikuu vya kilimo
ili kuleta tija ya kilimo katika sekta hiyo na Serikali yake itakuwa na
mkakati mahsusi wa kutoa elimu na mitaji kwa wakulima wanaofanya kilimo
chenye tija na kilimo cha kujikimu.
Katika afya, Malupu alisema kuwa atahakikisha suala la afya linasimamiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja kuwapatia wazee huduma bure na kwamba zahanati, vituo vya afya na hospitali zinapatiwa vifaatiba vya kutosha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Katika afya, Malupu alisema kuwa atahakikisha suala la afya linasimamiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja kuwapatia wazee huduma bure na kwamba zahanati, vituo vya afya na hospitali zinapatiwa vifaatiba vya kutosha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Malupu
pia alizungumzia wananchi wanaoishi katika visiwa vya Ukerewe mkoani
Mwanza na Mafia mkoani Pwani kuwa wamesahaulika, hivyo akiteuliwa na
baadaye kuchaguliwa atahakikisha anakifanya kisiwa cha Ukerewe kuwa mkoa
unaojitegemea ili kuwapunguzia wananchi umbali wa kufuata huduma
Mwanza.
“Wananchi
wa Visiwa vya Mafia na Ukerewe wanakabiliwa na changamoto za
upatikanaji wa huduma za kimkoa kutokana na mazingira ya kijiografia na
wamesahaulika kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Katika
hotuba yake hiyo, Malupu aliwataka vijana kutokata tamaa na kujitokeza
kugombea nafasi za udiwani, ubunge na urais pamoja na kujiandikisha
katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kutumia haki hiyo ya kikatiba
kwa kupiga kura.
Michezo
Akizungumzia
uboreshaji wa sekta ya michezo, Malupu alisema atahakikisha anaanzisha
vituo vya kulea vipaji katika mpira wa miguu vitakavyowawezesha vijana
kuibua vipaji na kuwapa elimu ya msingi kuhusu mpira wa miguu ili kuinua
soka la Tanzania. Pia, aliahidi kuboresha sekta ya filamu na muziki kwa
ujumla kwa kuwawekea vijana utaratibu maalumu ili waweze kujitengenezea
ajira za kudumu.
Polisi na nyumba
Aliahidi
kulipatia Jeshi la Polisi nyumba za shirika la nyumba ili kuondokana na
wanazokaa ambazo hazilingani na hadhi walionayo... “Nia yangu ni
kuhakikisha askari polisi wanakaa katika mazingira salama na yenye hadhi
yao siyo kama ilivyo sasa,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni