Juma Nature akitumbuiza kwenye viwanja vya Dar Live.
Nature ameiambia Bongo5 kuwa ni kutokana na chuki za watu wachache, uwezo wake unasahaulika.
“Japokuwa kuna watu wanaleta figisu figisu kutaka kunishusha kimuziki, najua jibu wamepata,” amesema Nature.
“Weekend iliyopita nimewafundisha watu nini maana ya kuwa mkongwe,
hili ni funzo kwa underground wote wajifunze wanatakiwa wafanye nini
kwenye muziki wao ili waendelee kuishi kwenye maisha ya watu.
Kinachofuata sasa hivi ni tour ya muziki wangu, nitazunguka katika mikoa
mbalimbali kuzungumza na mashabiki wangu pamoja na kufanya show, pia
kupitia show zangu za mikoani underground watapata nafasi ya kuperform.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni