Social Icons

Jumapili, 31 Mei 2015

Wasira Alipuka,Ampiga Kijembe Kiaina Lowasa,Atangaza Nia Ya Kwenda Magogoni





Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, amnabe pia ni Mbunge Bunda mkoani Mara, Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia baadae mwaka huu.

Katika hotuba yake ya takribani dakika 60 mh WASIRA ametumia muda mwingi kukemea vitendo vya rushwa hiuku akiwahmiza wananchi kumchagua kiongozi ambaye hatawaibia mali zao na badala yake wamchague mtu ambaye atawatumikia watanzania.


Amesema kuwa kiongozi anayekuja mbele za watu na kusema anaichukia ruswa wananchi wamwangalie usoni kama kweli anamaanisha anachoklisema au anasema kama fashion kwa sababu ameambiwa akisema anachukia rushwa atachaguliwa.

Amesema kuwa yeye ni kiongozi ambaye tangu tanzania imeanza kukumbwa na kashfa za wizi wa mali za umma hajawahi kutajwa wala kuhisiwa katika wizi huo hivyo anadhani yeye ni msafi na anafaa kuiongoza tanzania kwa miaka miktano ijayo

Wasira ametangaza siku moja baada ya Kada wa CCM na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kulitika jiji la Arusha wakati akitangaza nia kama hiyo.Miongoni mwa makada wa CCM ambao wanatarajiwa kutangaza nia kama ya Lowassa na Wassira ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba atakae tangaza nia hiyo baade leo, Charles Makongoro Nyerere, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, na makada wengine wengi wa chama hicho wametajwa kuwania nafasi hiyo.Wasira akitangaz nia hiyo hii leo katika Ukumbi wa BOT jijini Mwanza amesema yeye kauli mbiu yake ni Uadilifu.

Wasira Atangaza Nia Ya Kwenda Ikulu Ahimiza Uadidilifu

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, ambae pia ni Mbunge wa Bunda mkoani Mara, Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia baadae mwaka huu.

Wasira ametangaza siku moja baada ya Kada wa CCM na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kuliteka jiji la Arusha wakati akitangaza nia kama hiyo.

Miongoni mwa makada wa CCM ambao wanatarajiwa kutangaza nia kama ya Lowassa na Wassira ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba atakae tangaza nia hiyo baade leo, Charles Makongoro Nyerere, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, na makada wengine wengi wa chama hicho wametajwa kuwania nafasi hiyo.

Wasira akitangaza nia hiyo hii leo katika Ukumbi wa BOT jijini Mwanza amesema yeye kauli mbiu yake ni Uadilifu.

Magazeti Ya Leo Jumapili Mei 31,2015 Yako Hapa


Diamond Platnumz, Khadija Kopa,Tunda Man, Makomando, Walter Chilambo Kwenye Stage Moja Ya Lowassa Arusha Jana


  

                             Diamond 


MAY 30 2015 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha ilikuwa siku ambayo Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa alitangaza rasmi kwamba ataomba kibali cha CCM ili agombee Urais wa TZ mwaka huu. 


Baada ya hapo watu wakaigeukia stage ya burudani ambapo ilikuwepo list pia ya mastaa wa Bongo Fleva ambao walipiga show ya nguvu. 



                      Khadija Kopa 


 

 

Walter Chilambo 

 

  

 

  

Makomando 


 

 

Tundaman 

 

  

 

Jumamosi, 30 Mei 2015

Waziri Lukuvi Aweka Jiwe La Msingi Nyumba 50 Za Gharama Nafuu Za Shirika La Nyumba La Taifa Wilayani Kahama





Hizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga.
 Mei 29,2015 Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba hizo zilizojengwa na NHC wilayani Kahama mkoani Shinyanga 

Kaimu mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki kutoka Shirika la nyumba la taifa Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa waziri Lukuvi kuhusu mradi huo wa nyumba 50 wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.

Mradi huo wa nyumba 50 utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.1 na kila nyumba ina vyumba vitatu. 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akikata utepe,kulia kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwa ndani ya moja ya majengo hayo,wa kwanza kushoto ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi 

Wa pili kulia ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akitoa maelekezo kwa waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50 yaliyojengwa na NHC

Meza kuu-Lengo la NHC kujenga nyumba ni kuleta mvuto kwa miji yetu,kupandisha hadhi ya maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na gharama nafuu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Kahama mjini James Lembeli 

Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson akizungumza eneo la tukio.Alilipongeza shirika la nyumba la taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara,huku akipongeza pia kitendo cha NHC kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika halmashauri za wilaya
Eneo la tukio


Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akizungumza eneo la tukio,alisema mradi huo wa nyumba za Kahama ni muendelezo wa utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini ikiwa ni miongoni mwa maeneo 29 ya halmashauri mbalimbali za miji.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi, alisema mradi huo wa umetengeza ajira za moja kwa moja 290,ajira shirikishi 145,makazi ya watu 300 na utanufaisha wananchi wa Kahama wakiwemo wafanyabiashara. 


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama.
Tunamsikiliza waziri Lukuvi....

Waziri Lukuvi pamoja na mambo mengine alizitaka halmashauri za wilaya kupima maeneo ya miji na kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango ya miji vizuri.


Wananchi wakimsikiliza waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi,ambaye alisema wananchi watakaonunua nyumba za shirika la nyumba la taifa hivi sasa kuna utaratibu wa kupatiwa hati miliki hata kama nyumba iko juu ya ghorofa ili kuwarahisishia kupata mahitaji mengine muhimu ikiwemo mikopo.

Tunafuatilia kinachoendelea.....




Kundi la sanaa la Makhirikhiri wa Kahama wakitoa burudani

Nyumba moja inauzwa shilingi milioni 49 na tayari watu mbalimbali wamejitokeza kununua nyumba hizo za kisasa


Kundi la Makhirikhiri likitoa burudani


Kiongozi wa kundi la sanaa la Makhirikhiri Kahama akishikana mkono na viongozi akiwemo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi


Wananchi wakiwa eneo la tukio

Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.



Wananchi wakiwa eneo la tukio