Diamond Platnumz na P-Square wako njiani kusumbua amani katika kiwanda cha muziki barani Afrika.
Collabo yao ambayo tayari imekwishakamilika inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.Diamond ameshare picha akiwa studio na mapacha hao wa kundi hilo, Peter na Paul Okoye ambayo huenda ni ya wiki kadhaa zilizopita.
“Tafadhali mkiwa Tayari naomba mnambie niiachie, DIAMOND ft P-SQUARE, #MISISAIZIYAKONTAKUPWELEPWETABURE @rudeboypsquare @peterpsquare,” ameandika Diamond.
Si Diamond pekee mwenye furaha na collabo hiyo, bali na P-Square pia.
Peter amepost pia picha hiyo na kuandika: My African people, you asked for it and it’s coming to you soon,” huku Paul akiandika: Hmmmmm…..something is cooking.”
Mashabiki wao wamepokea habari hizo kwa furaha kubwa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni