Social Icons

Jumanne, 26 Mei 2015

The King Of All Bongo Social Media Network:- BASATA Wapo Out Of The Control Wamevuruga Tunzo Za Watu Juzi Live!!!


 

 

Serikali Iwatupie Jicho Kali BASATA:- They are Out Of The Control & Incompetence!!

- Well, nilidhani BASATA inatakiwa kuinua Vipaji vya Wasanii na kuvikuza vipande juu zaidi lakini wanachokifanya sasa hivi sio kabisa ni wakati muafaka wa Serikali kuwatupia jicho kali na kuwarekebisha sasa na mapema kabla hawajafika mbali na kuvuruga sanaa nchini, kwa mfano:-

1. MISS TANZANIA:- BASATA wameifungia Miss Tanzania kwa sababu ambazo kama ni kweli zipo zinawahusu tu Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania lakini haziwahusu Vijana wadogo wa kike ambao hawana kosa lolote, sasa BASATA wameifungia Miaka Miwili nia na madhumuni ni nini hasa? Kuwakomoa Viongozi au Wasichana? Halafu Taifa linafaidikaje na kuwafungia Vijana wadogo kufanya mashindano ambayo kabla hayajafungiwa yamewaletea mafanikio makubwa kimaisha baadhi ya washiriki, Wasichana kama Hoyce Temu, sasa hivi ni Balozi wa Umoja wa Mataifa na pia ni mfanya biashara mkubwa anayemiliki Club maarufu ya 327 hapa mjini wala sio siri haya mafanikio yake kimaisha yametokana na kushinda kwake haya mashindano, wapo wengi kama Miriam Odemba ambaye sasa anaishi Paris, France anakofanyia kazi zake za Modelling na yeye alitokea kwenye haya haya mashindano, Millene Magese, Faraja Kota, Klyn, I mean I can go on and on wote wametokea kwenye haya mashindano.

- Majuzi Msichana mdogo Doris Mollel amefungua Foundation ya kusaidia watoto premature, uzinduzi umefanyika Kempisk Hotel na alichangiwa karibu Shillingi Millioni 100 now huyu msichana amepitia mashindano haya haya mwaka jana tu, I mean leo kuna wasichana wengi sana ambao walikuwa wanasubiri na wao wapate nafasi ya kushiriki haya mashindano na wao watimize ndoto zao, ni kawaida ya mataifa yote huru Duniani kuwaruhusu wananchi wake kutumia all available resources kujisongeza mbele kimasha, sasa kwa kuwafungia miaka 2 exactly BASATA wana accomplish what?

2. TUZO ZA WATU:- Majuzi BASATA wamesimamia hizi tuzo ambazo matokeo yake yalikuwa ni maajabu ya Dunia, kwenye TUZO zote Duniani za WAsanii hata zikiwepo kura bado lazima kuwepo na vigezo vingine, kwa mfano kura zinatakiwa kushika kama 30% 50% Ubora wa kazi za Msanii 20% ni kukubalika kwa Msanii ndani na nje ya Nchi, lakini haiwezekani ukahukumu kazi za Msanii kwa kutumia kura 100% that is the biggest joke of my life, I m,ean kuna makosa mengi sana yamefanyika kwenye hizo Tuzo na huwezi kusema ni Tuzo ndogo no way ikishawajumlisha WAsanii maarufu kama Diamond, Mzee Majuto na JB hizo ni Tuzo kubwa sana na ni muhimu kwenye CV ya Msanii,

- CATEGORY ya Blog:- Seriously kama kweli BASATA na watayarishaji wa zile TUZO wangekuwa serious hakuna Blog au website Tanzania inayoizidi Jamiiforums nasema hakuna, Jamiiforums ndiyo website peke yake inayopitiwa na Viewers wengi with straight numbers bila kurudia rudia, kwa mfano ukiona kuna website namba zake zinaonyesha imepitiwa na viewers Laki Mbili kwa siku maana yake ni kwamba wamepitia Viewers Laki moja wakarudia rudia kuingia na kutoka, lakini only Jamiiforums ndiyo ina wasiojirudia staright in numbers kama Laki Mbili ni hizo hizo Mbili sasa leo hata kwenye nomination haikuwemo, WHY?

- MWANAMUZIKI MWANAUME ANAYEPENDWA TANZANIA KULIKO WOTE:- Please nani Tanzania ya leo anayeweza kumshinda Diamond? I mean eti ameshindwa kwa sababu hakupata kura, hizi kura zinatusumbua sana Tanzania kila siku kwenye siasa ni ugomvi kisa kura leo unazileta tena kwenye kuamua ubora wa kazi za msanii? That is a shame now BASATA hawawezi kukwepa hii lawama kwa sababu walikuwepo na ni lazima walihusika, watayarishaji sio tatizo sana lakini tatizo ni kushiriki kwa BASATA kwenye zile Tunzo kunawabana sana na FULL RESPONSIBILITY ya kila kilichofanyika kwa uzuri na ubaya, uzuri ni kwamba ni muhimu sana kuwepo kwa hizi Tunzo lakini ubaya ni kwamba BASATA haina watu competent enough wa kusimamia Vipaji vya wasanii,

- BASATA wanahitaji kupunguzwa nguvu now kabla hawajaharibu kabisa hii field ya Sanaa, cause tukiendelea na huu mfumo wa kupiga kura kuhukumu kazi za wasanii maana yake ni kwamba tunafungua miaanya wa watu kuanza kuvuta rushwa tu, Msanii afanye kazi zake zionekane lakini tusimpe mzigo wa kuanza kutafuta kura za kuhukumu ubora wa kazi zake hapana, kipaji chochote kinatakiwa kuhukumiwa na matokeo ya kazi zake mbele ya jamii.

- Now kwa hayo yote ninarudia tena kusema Diamond hakushinda kura kwa hiyo sio MSanii anayependwa sana na jamii ni njia rahisi sana ya kuua vipaji vya sanaa yetu, ninasema BASATA wamekosea na wanatakiwa kuangaliwa na Serikali now kabla hawajatufikisha kurudi kule kule tulikotoka kwenye kushangilia kina Kandabongoman MWanamuziki ambaye huko kwao hawezi kupiga dansi la peke yake akajaza watu mpaka aje Tanzania, siku hizi tumepigana tumeinua Vipaji vyetu ndio maana hawa wageni hawaji tena yale mambo ya bendi za Wakongo kusumbua hapa mjini hamna tena, sasa wanakuja BASATA na kutaka kuivuruga Sanaa, SErikali ni lazima iingilie kati tena sasa!!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni