Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameitisha mkutano
wa wakuu wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili kujadili
mgogoro unaoikabili Burundi.
Rais Kikwete ameitisha mkutano huo wakati Burundi ikiripotiwa kuwa
katika vurugu zinazotishia hali ya usalama, hasa kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Kiduru wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) amesema kuwa, kuna haja ya kufanyika mkutano huo kwa
ajili ya kujadili mgogoro wa kisiasa unaoikabili Burundi.
Rais Kikwete amesema kama ninavyomnukuu: “Tumekubaliana kuwa sisi ndani
ya EAC yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi yenyewe tukutane
Dar es Salaam, Jumatano ya keshokutwa, ili tujadiliane jinsi gani ya
kuwasaidia ndugu zetu wa Burundi kuandaa uchaguzi wao kwa mafanikio,
wakihakikisha kuwa nchi yao inabakia na umoja, utulivu, usalama na amani
bila misukosuko isiyokuwa na sababu. Wakati huo huo, wimbi la wakimbizi
wa Burundi wanaoingia Tanzania linazidi kuongezeka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni