Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza,
amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji
mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita.
Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara.
Mapema
hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura,
kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni