Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah
Mwambene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) ndani ya ukumbi wa
Idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Msahuri,kumbukumbu za ukombozi wa Barani Afrika,Daniel Ndagala, Mshauri
na mtafiti UNESCO Phelippe Roisse na wa mwisho ni Dinah Mumbaga
Mtafiti na mshauri wa UNESCO.(Picha na Avila Kakingo).
WAZIRI
wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh.Bernard Membe
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki
ya Ukombozi Barani Afrika, maadhimisho hayo yatazinduliwa katika ukumbi
wa mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Mei 25 mwaka
huu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana
na maadhimisho hayo ya wiki ya Ukombozi Barani Afrika.
Mwambene amesema kuwa Serikali
ikishirikiana na shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watazindua Mradi wa Nyaraka za Urithi wa
Tanzania(TAHAP), ambao ukikamilika utakuwa unaweka na kutunza
kumbukumbu za nyaraka mbalimbali zinazohusu Ukombozi Barani Afrika.
Amesema
kuwa miongoni mwa matukio muhimu katika maadhimisho hayo ni pamoja na
mdahalo unahohusu mchango wa vyama vya siasa katika harakati za
ukombozi utakaoongozwa na Dk. Salim Ahmed Salim, Profesa Issa Shivji
pamoja na Mh.Ibrahim Kaduma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni