Hatimaye ni kama Rais Kikwete amepuuza kilio hicho na kusiani Mswaada
huo na kuwa Sheria Rasmi na kuanzia kutumika kuanzia kesho.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akithibitisha kusainiwa kwa Mswaada huo na kuwa sheria Rasmi na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Prof. Makame Mbarawa leo jijini Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari ambapo amesema Baada ya Mswaada huo kupitia sehemu
mbali mbalina kuonekana hauna Tatizo lolote ndio ukamfanya Rais Kikwete
kusiani Mswaada huo.
Waziri Mbarawa amesema Sheria hiyo itasaidia kupunguza Makosa mbali
mbali ya watu wanaofanya kwa Makusudi kwenye Mtandao Jambo ambalo
anadai italiweka Taifa salama na kuondokana na Tabia iliyojijengeka kwa
Baadhi ya watu kuandika Habari na kusambaza Taarifa za upotoshaji kwenye
Mitandao ya Kijamii.
Pamoja
na hayo Waziri Mbarawa amesema kwa sasa baada ya Rais Kikwete kusaini
hatua inayofuata ni kazi ya Wizara hiyo kuwaelimishwa wananchi kuijua
sheria hiyo ili kuanza kutimika Rasmi.
Aidha,Waziri huyo amesema kwa wale wadau mbali mbali wa Masuala ya
Habari na wanasiasa pamoja na Wanaharakati ambao walikuwa wanaubeza
Mswaada huo,wanatakiwa kuwasilisha hoja zao kwenye Wizara yake ili hatua
zichukuliwe kwenye Vipengele ambavyo Wizara hiyo itaviona labda
vitakuwa na Utata .
Vilevile akawataka Watanzania kuipokea sheria hiyo kwa Manufaa makubwa
kutokana na Uharifu wa Mitandao hivi sasa ambao ulikuwa unawasumbua.
Kusaniniwa kwa Msaada kunatafsiliwa na wadau mbali mbali wa Masuala ya
Habari nchini ni kama umeendelea kunyonga Uhuru wa Habari nchini
kutokana na Sheria hiyo kuwepo na Vifungu Kandamizi kwa watu wanaotoa
Taarifa kwa Umma kwa njia ya Mitandao.
Wadau mbali mbali wa masuala ya Habari waliokutana tarehe 2 ya mwezi
huu Mkoani Morogoro siku ya Vyombo Vya Habari Duniani walimtaka Rais
Kikwete kutosaini Mswaada huo kwani utaiweka Njia panda Taifa na
wakadai Uhuru wa Habari unazidi wambwa Msalabani kutokana na Vipengele
vilivyopo kwenye Sheria hiyo mpya.
Wanasheria wananena
Wanasheria
Mmoja Maarufu hapa Jijini aliyezungumza na Mtandao huu amesema kitendo
cha Rais kikwete kusaini Mswaada huo na kuwa sheria ni kama kuua Rasmi
Uhuru wa kutoa habari na kupata Habari.
“kusema
kweli Rais Kikwete amenisikitisha sana kusaini Mswaada wenye utata leo
Rais Kikwete wakati anaingia madarakani alitoa uhuru mkubwa wa kujieleza
na kutoa maoni inakuwaje sasa anakubali kusaini mswaada wenye utata
kama huu ambao unamkosa chungu mzima”amesema Mwanasheria.
Gwaji huyo wa Sheria alizidi kuongea kwa Uchungu amesema kwa sasa Jinsi
hali anavyoiona basi watanzania wengi wajiadhali kuishia magerezani
kutokana na kuwa na Vipengele anavyodai vina utata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni