BAADA
ya Kimya kizito hatimaye Edward lowassa, naweza kusema ameamua kuvunja
ukimya huo na kuibuka kutamka wazi wazi kwamba anaitaka Nafasi ya Urais
ndani Chama cha Mapinduzi CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa hapo baadae mwaka
huu .Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kuibuka kwa Lowassa ambaye ni Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa Kashfa ya
Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound ,kuna kuja siku moja kupita
baada ya CCM kutangaza rasmi tarehe kwa makada wake kuanza kuchukua Fomu ya
kuwania kwenye uongozi mbali mbali kwenye Uchaguzi mkuu hapo baadae .
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli CCM ameisema kauli hiyo leo
Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema yupo Vizuti
katika kuwania nafasi ya Urais na anatarajia kutangaza rasmi hapo
Jumamosi ya wiki hii.
“Nataka kuwahakikishia nyinyi na watanzania niko vizuri kwa teyari kwa
chochote na nipo sawa kuwania nafasi ya Urais ambayo natarajia kutangaza
hapo Jumamosi”amesema Lowassa.
Lowassa ambaye pia ni Mwenyikiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano kimataifa amesema kutokana na tatizo la kubwa la Vijana
kukosa Ajira ndio miongoni mwa sababu iliomfanya ajitose kwenye Nafasi
hiyo kubwa na uongozi wanchi.
“Tatizo
la Ajira ni Bomu ambalo linatarajia kuripuka na,kwakuwa wako vijana
wengi wamemaliza Vyuo vikuu hawana Ajira wapo mitaani unategemea
nini,wakati wenzetu katika nchi zilizoendelea katika kipindi cha Kampeni
wanaweka wazi mambo ya Ajira, na sio kuwekeza kwenye Kilimo Kwanza na
hata chama changu wanajua kwamba sera ya Kilimo kwanza siikubaliani nayo
unaitaji taifa liloendelea kwa kuwekeza kwenye Elimu.”
KUHUSU AFYA YAKE
Lowasa amesema kuhusu suala la Afya ni amedani ni chuki tu ipo kwenye Chama chake cha CCM.
“Kuna
chuki imeingia ndani ya chama chetu na mimi nasema chama chetu waweke
utaratibu wa kupima Afya ambao tunagombania nafasi ya Urais waweke
utaratibu wa kufanya hivyo na mimi nawahakikishia nipo vizuri”amesema
Lowassa.
KUHUSU KUHAMA CCM.
Lowassa
pia alizungumzia suala hilo ambalo mara kwa mara lilikuwa likiandikwa
kwenye magazeti ambayo yalikuwa yakidai endepo atakatwa jina lake ndani
ya CCM atajiunga kwenye Chama kipya cha kisiasa cha ACT-Wazaendo.
Ambapo lowassa amesema hawezi kuhama chama hicho kikongwe kilichopo barani Afrika.
“Kuhama chama sina mpango nimeamia CCM mwaka 1977 sijafanya kazi sehemu
popote zaidi ya CCM maisha yangu yote yapo CCM anayetaka nihame basi
ahame yeye”.
VIJEMBE KWA UTAWALA WA KIKWETE.
Sanjari
na kuweka mipango ya kuwaokoa Vijana pia Mwanasiasa huyo Mkongwe
akusita kutoa Vijembe kwa Rais anayemaliza mda wake Rais Jakaya kikwete
kwa kusema limefika hapo kwenye matatizo kutokana na kuwa kwa watendaji
wabovu wanaofanya kazi kimazoea.
KUHUSU MADAI ANAYODAI NI YA VISASI.
Lowassa
ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM amesema kuhusu Visasi
kwamba yeye ni ni Mkristo na hana Visasi na mtu yeyote.
“Mimi ni Mkristo hata bwana yesu alisema samehe mara sabini sina kisasi na mtu yeyote”
KUHUSU HALI YA UPINZANI.
Mbali na mambo hayo pia Lowassa amezungumzia hali ya vyama vya Upinzani na ameikitaka chama chake kisizubae.
“Nachoweza
kusema kwamba Upinzani umepata nguvu,mijini na Vijijini, sisi ni chama
kinachoshika Dola tusizubae na wenzetu wameanza pata nguvu
tusibweteke,maana wenzetu wamejiandaa vizuri,na sisi tunapaswa kujipanga
maana Vyama vya Ukombozi Afrika vimeondolewa kwahiyo tusijisahu maana
ukitoka madakani urudi”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni