Ripoti ya Forbes mwaka
2014 ilionesha P Diddy ameongoza kwenye list ya mastaa wa Hiphop wenye
utajiri mkubwa zaidi, akafuatia Hiphop star Dr. Dre, #3 akakaa Jay Z,
#4Birdman na #5 alikuwepo 50 Cent.. imetoka ripoti mpya, yes kuna
mabadiliko kwenye hiyo list mtu wangu.
Mpangilio wenyewe mwaka 2015 ni huu hapa.
No.5: Rapper Birdman,
mmoja ya members wa YMCMB. Utajiri wake kwa sasa unaonekana ni kama dola
Mil. 150 hivi. Mwaka 2014 alikuwa nafasi ya nne kwa utajiri wa dola
160, ni kama biashara ya muziki bado haijawa vizuri kwa upande wake
mwaka huu.
No.4: Rapper 50 Cent
yuko namba nne, utajiri wake ni dola Mil.155. Ripoti ya mwaka 2014
ilionesha alikuwa nafasi ya 5 na utajiri wake ulikuwa dola Mil. 140,
kapanda nafasi moja juu yani !!No.3: YES YES !! Ni Jay Z
mtu wangu, mwaka jana alikuwa nafasi hiyo hiyo ya tatu, utajiri wake
ulikuwa sawa na dola Mil. 550 na mwaka huu kiwango ni hicho hicho. Jamaa
ni mfanyabiashara wa ukweli, labda tusubiri kuona account zake benki
zikituna zaidi baada ya kuzindua biashara ya Tidal !!No.2: Dr. Dre, jamaa ni
rapper, producer na mjasiriamali pia !! Biashara ya headphone za ‘Beats
by Dre’ ni kitu kingine kikubwa kilichomuingizia pesa nyingi sana kabla
hajauza mradi huo kwa Kampuni ya Apple. Utajiri wake ni dola Mil. 700,
mwaka jana alikuwa dola Mil.550No.1: Hajatoka kwenye
hii nafasi ya kwanza ambayo hata mwaka 2014 alikuwa hapo pia, jamaa
anabadilisha majina kila wakati !! Diddy ana utajiri wa dola Mil.735..
mwaka jana alikuwa na utajiri wa dola Mil.700.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni