Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana,
Kwa ufupi
- Adai CUF imefanya utafiti na kubaini
kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar iliandikisha marehemu na watoto wakapiga
kura Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ametoa tuhuma nzito dhidi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) akidai kuwa iliandikisha na kuruhusu wapigakura wasiostahili zaidi ya 10,000 kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, wakiwamo marehemu 8,507.Maalim Seif aliyewania urais wa Zanzibar katika uchaguzi huo na kushindwa ikiwa ni mara ya tano na wagombea wa CCM, alitoa tuhuma hizo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akisema wapigakura hao wasiostahili, bado wapo kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura la Zanzibar.Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alikuwa akizungumzia utafiti wa Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Zanzibar uliofanywa kati ya Agosti 2014 hadi Machi 2015. Alieleza pia kwa nini hakulalamika wakati huo na badala yake akakubali matokeo.Kwa nini alikubali matokeo?“Ni ukweli usiopingika kwamba uchaguzi huo ulikuwa na mapungufu lukuki lakini mawakala wetu hawakuwa na vithibitisho, hatukuweza kupinga matokeo yale kwa sababu hatukuwa na uthibitisho wowote.”Aliongeza, “Hivi unaweza kusema matokeo siyo ya haki wakati huna uthibitisho? Lakini utafiti huu umeweka wazi mambo yote yaliyofanywa nyuma ya pazia kwenye uchaguzi uliopita, kwa hiyo sasa tuna uthibitisho wa kutosha.”Kiongozi huyo alisema endapo kasoro hizo zikifanyiwa kazi, Rais wa sasa, Dk Ali Mohamed Shein ajiandae kisaikolojia kuwa makamu wa rais wakati yeye akiwa Rais baada ya uchaguzi ujao.Kasoro za uandikishajiKwa mujibu utafiti huo, ZEC iliandikisha katika daftari hilo wapigakura wenye umri chini ya miaka 18, ambao si wakazi katika maeneo waliojiandikisha na waliotumia majina na picha ambazo siyo zao.Alisema licha ya baadhi ya watu hao kuwa marehemu na wengine wasiokuwa na sifa, bado hawajafutwa kwenye daftari hilo tangu 2010 na majina yao yatatumika kupiga kura mwaka huu.Akizungumza kwa kujiamini huku akitabasamu, Maalim Seif alisema utafiti huo unaonyesha kuwa kuna zaidi ya watu 10,000 ambao waliandikishwa kinyume na sheria na kwamba walipiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2010.Akitoa mfano huku akirejea utafiti huo, Maalim Seif alidai kwamba katika Jimbo la Donge, ZEC iliandikisha watoto 463 ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 na kwamba walipiga kura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni