Hizi ni miongoni mwa
nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa
(NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya
Mji Kahama mkoani Shinyanga.
Mei 29,2015 Waziri wa Ardhi ,Nyumba na
Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika
nyumba hizo.
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka
jiwe la msingi katika nyumba hizo zilizojengwa na NHC wilayani Kahama
mkoani Shinyanga
Kaimu mkurugenzi wa
Uendelezaji Miliki kutoka Shirika la nyumba la taifa Haikamen Mlekio
akitoa maelezo kwa waziri Lukuvi kuhusu mradi huo wa nyumba 50 wilayani
Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa
kukamilika mwezi Desemba 2015.
Mradi huo wa nyumba 50 utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.1 na kila nyumba ina vyumba vitatu.
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akikata utepe,kulia kwake
ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwa ndani ya moja ya
majengo hayo,wa kwanza kushoto ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la
nyumba la taifa Felix Maagi
Wa pili kulia ni kaimu
mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akitoa
maelekezo kwa waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50
yaliyojengwa na NHC
Meza kuu-Lengo la NHC
kujenga nyumba ni kuleta mvuto kwa miji yetu,kupandisha hadhi ya maeneo
lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na gharama
nafuu
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiteta jambo na mbunge wa
jimbo la Kahama mjini James Lembeli
Mkuu wa wilaya ya Kahama
Benson akizungumza eneo la tukio.Alilipongeza shirika la nyumba la
taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara,huku akipongeza pia kitendo
cha NHC kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika
halmashauri za wilaya
Eneo la tukio
Kaimu mkurugenzi mkuu wa
Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akizungumza eneo la
tukio,alisema mradi huo wa nyumba za Kahama ni muendelezo wa utekelezaji
wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini ikiwa ni
miongoni mwa maeneo 29 ya halmashauri mbalimbali za miji.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa
Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi, alisema mradi huo wa umetengeza
ajira za moja kwa moja 290,ajira shirikishi 145,makazi ya watu 300 na
utanufaisha wananchi wa Kahama wakiwemo wafanyabiashara.
Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa
Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na shirika la
nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula
wilayani Kahama.
Tunamsikiliza waziri Lukuvi....
Waziri Lukuvi pamoja na
mambo mengine alizitaka halmashauri za wilaya kupima maeneo ya miji na
kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya
ardhi na kuweka mipango ya miji vizuri.
Wananchi wakimsikiliza
waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William
Lukuvi,ambaye alisema wananchi watakaonunua nyumba za shirika la nyumba
la taifa hivi sasa kuna utaratibu wa kupatiwa hati miliki hata kama
nyumba iko juu ya ghorofa ili kuwarahisishia kupata mahitaji mengine
muhimu ikiwemo mikopo.
Tunafuatilia kinachoendelea.....
Kundi la sanaa la Makhirikhiri wa Kahama wakitoa burudani
Nyumba moja inauzwa shilingi milioni 49 na tayari watu mbalimbali wamejitokeza kununua nyumba hizo za kisasa
Kundi la Makhirikhiri likitoa burudani
Kiongozi wa kundi la sanaa la Makhirikhiri Kahama akishikana mkono na viongozi akiwemo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni