Social Icons

Jumatano, 20 Mei 2015

Wema Na Aunt Ezekiel Vilio Tupu, Ni Baada Ya Kula Viapo Vya Kutozikana


Baada ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.

 
Aunt Ezekiel akimbembeleza Wema baada ya kupatanishwa. 


Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.

Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.

Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.

Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo. 

 
Wakiwa na rafiki yao Daudi Mambya anayedaiwa kuwapatanishwa. 


 
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.” 


Wema alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni