Hata hivyo hali bado ni ya kutatanisha, huku Ikulu ya
nchi hiyo ikiwa imekanusha kutokea kwa mapinduzi hayo kupitia mtandao wa
Twitter, ikisema yameshindwa.
Jenerali Godefroid Niyombare, mkuu wa zamani wa ujasusi
nchini humo aliye na ushawishi mkubwa ametangaza mapinduzi hayo saa chache
baada ya viongozi wa nchi jirani za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana jijini
Dar es Salaam Tanzania kuzungumzia hali halisi ya Burundi.
" Rais
Nkurunziza ameondolewa madarakani, serikali imevunjwa, watu wote wanaombwa
kuheshimu maisha na mali vya wengine," alisema Jenerali General Niyombare
kupitia chombo kimoja cha habari cha kibinafsi nchini humo.
Kwa sasa takriban watu 20 wameuwawa huku wengine wengi
wakijeruhiwa tangu katikati ya mwezi wa Aprili wakati chama tawala cha CNDD FDD
kilipomuidhinisha Nkurunziza kama mgombea wao wa Urais katika uchaguzi
uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni 2015.
Mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama
nchini humo yamezua wasiwasi kwamba huenda ghasia zikatokea tena katika nchi
hiyo ya Afrika ya kati ambayo bado inajikwamua kutoka miaka kumi na mitatu ya
vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka wa 2005.
Lakini huku
viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wakitafuta ufumbuzi wa mgogoro wa
Burundi raia wa nchi hiyo takriban 50,000 wameripotiwa kuitoroka nchi hiyo na
kukimbilia nchi jirani tangu kuanza kwa machafuko.
PICHA NA :-BBC SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni