Social Icons

Ijumaa, 15 Mei 2015

Waziri Nyalandu Ajibu Tuhuma Alizopewa Na Mbunge Nassari Bungeni.

 

       Tamko la Mhe.Nyalandu kuhusu shutuma za Mbunge Mhe.Nassari

“Nimesikitishwa sana na kauli ya Mhe. Joshua Nassari ambayo ameongea kwa kudhalilisha utendaji wangu serikalini.  

Naomba Mh.Nassari afahamu kuwa kunikashifu pasipo kueleza masuala ya kisera  au ya kiutendaji ni kupungukiwa na busara ya kawaida kwa kiongozi aliyepaswa kuwa wakilisha wapiga kura wake kwa hoja. Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mhe.Nassari aliniita Jimboni kwake Arumeru Mashariki akiniomba nitatue tatizo lililohusu wananchi wa jimboni kwake waliokuwa wanahitaji matibabu katika hospitali ambayo  ilikuwa sharti upitie ndani ya hifadhi iliufike kutibiwa.


Nilikwenda kuwaona wagonjwa na kuitembelea hospitali hiyo na kulitatua tatizo hilo siku hiyo hiyo.  Kwangu kama Waziri, haliku wasuala  la  kufanyia siasa afya za Watanzania, pamoja na yeye kuwa Mbunge wa upinzani.
Nilimheshimu na kukubali wito wake kwaniabaya wananchi.  Nimewatembelea na kuwatia moyo maaskari wetu nchi nzima na kuwapelekea vitendeakazi.

Nimefurahi pamoja nao na kulia pamoja nao. Nimeenda kuwafariji familia zawapiganaji wetu waliopoteza maisha kwa kuuawa wakilinda raslimaliza Taifa, watu ambao Mhe.Nassari anawabeza.Tumepambana naujangili na tunaendelea kuushinda. Tumeleta magari, silaha,  ndege, helicopters, na raslimali nyingi ilikulinda raslimali za Taifa.  Busara  haisomewi ilani kumshukuru Mungu akusaidie kujua matumizi ya ulimi. Nimesikitishwa sana na kauli za uongo na kuzusha za Mhe.Nassari.
Imeandikwa, usimsingizie jirani ya kouongo.”

Mh. LazaroNyalandu.


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni