Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika, amnabe pia ni Mbunge Bunda mkoani Mara,
Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia
baadae mwaka huu.
Katika
hotuba yake ya takribani dakika 60 mh WASIRA ametumia muda mwingi
kukemea vitendo vya rushwa hiuku akiwahmiza wananchi kumchagua kiongozi
ambaye hatawaibia mali zao na badala yake wamchague mtu ambaye
atawatumikia watanzania.
Amesema
kuwa kiongozi anayekuja mbele za watu na kusema anaichukia ruswa
wananchi wamwangalie usoni kama kweli anamaanisha anachoklisema au
anasema kama fashion kwa sababu ameambiwa akisema anachukia rushwa
atachaguliwa.
Amesema
kuwa yeye ni kiongozi ambaye tangu tanzania imeanza kukumbwa na kashfa
za wizi wa mali za umma hajawahi kutajwa wala kuhisiwa katika wizi huo
hivyo anadhani yeye ni msafi na anafaa kuiongoza tanzania kwa miaka
miktano ijayo
Wasira
ametangaza siku moja baada ya Kada wa CCM na Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kulitika jiji la Arusha wakati
akitangaza nia kama hiyo.Miongoni mwa makada wa CCM ambao wanatarajiwa
kutangaza nia kama ya Lowassa na Wassira ni Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Mchemba atakae tangaza nia hiyo baade leo, Charles Makongoro
Nyerere, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, na makada wengine wengi wa
chama hicho wametajwa kuwania nafasi hiyo.Wasira akitangaz nia hiyo hii
leo katika Ukumbi wa BOT jijini Mwanza amesema yeye kauli mbiu yake ni
Uadilifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni