Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.
Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili
vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata
watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa
huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria
wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi
pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya
magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata
watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa
hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za
ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao
mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua
biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji
mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa
amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko
yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo
asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la
nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu
alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na
kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula
nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya
kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni