Rais Dk. Jakaya Kikwete.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana
Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma,
kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.
Aidha, Rais Kikwete
amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi
katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.
Katika mabadiliko hayo,
Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya
Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa
wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni
Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka
huu, 2015.
Wakuu wengine wa wilaya
ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka
Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Dkt.
Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma, Agnes
Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwenda Wilaya
ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi,
Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.
Wengine ambao
wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda
Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda
Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa
Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro John
Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na
Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya
Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Mei, 2015
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni