Baada
ya picha chafu za Shilole kusambaa mtandaoni hadi kupelekea BASATA
kumuandikia barua ya onyo, muimbaji huyo wa ‘Nakomaa na Jiji’ amevunja
ukimya.
Shilole
amesema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani wakati
akitumbuiza Ubelgiji hivi karibuni, kwa sababu ilikuwa bahati mbaya na
hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.
Shishi
ambaye ni mama wa watoto wawili amesema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku
hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza
akiwa ameivaa.
“Kiukweli
kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe
naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu
ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri […] yaani hii
nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati
niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion .” Alisema Shishi kupitia 255 ya Clouds Fm.
Ameongeza
kuwa amesikitishwa na mtu aliyempiga picha hizo na kuamua kuzisambaza
mtandaoni bila kujua kuwa itamuumiza yeye kama mwanamke.
“Nasisitiza
tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika
kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria
kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi
nitaumia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu
mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje nani huyo mtu aliyefanya hivyo, sio
mtu mzuri.”
Kuhusu
kama amepokea barua ya kuitwa kujieleza kutoka BASATA, Shishi amesema
kuwa hajapokea barua hiyo kwasababu bado yuko Ubelgiji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni