skip to main |
skip to sidebar
Mafuriko Dar es Salaam Ni Ushahidi Wa Athari Za Mabadiliko Ya Tabianchi
Hali ya mafuriko kama inavyoonekana eneo la Jangwani katika kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam, Tanzania.
Mvua zinazoendelea kunyesha nakusababisha mafuriko na hasara kubwa
jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini zimetajwa kuwa ni moja ya
ushahidi wa udhaifu wa miundombinu ya kweza kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi ambayo ni janga kubwa duniani kwa sasa. Haya
yalisemwa na FORUMCC; shirika linalijihusisha na masuala ya mabadiliko
ya Tabianchi.
Watu zaidi ya 12 wameripotiwa kupoteza maisha mpaka sasa kutokana
mafururiko hayo ambayo yameibua hisia na maswali mengi kutoka kwa
wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wengi wakihoji nani wa
kulaumiwa kutokana na mafuriko hayo.
Afisa Miradi, Fazal Issa kutoka shirika la ForumCC ameitaka serikali na
watu binafsi kuchukua hatua thabiti katika kukabiliana na mafuriko haya
ambayo yanasababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa serikali na taasisi zake imekuwa na kawaida ya kuchukua
hatua mara baada ya madhara kutokea badala ya kuweka mikakati ya muda
mrefu ya kukabiliana na viashiria vya athari za mabadiliko ya tabianchi.
“Taasisi zenye majuku ya kutoa tahadhari na kushughulikia majanga hasa
ya mafuriko, mamlaka zinazohusika na ujenzi wa miundombinu katika jiji
la Dar es Salaam, ukusanyaji na utoaji wa taka zinapaswa kufanyakazi kwa
kushirikiana ili kutafuta suluhisho la kukomesha maafa haya kabla
hayajaleta athari kwa watu” alisema Issa.
Alisema hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwani utabiri wa Mamlaka ya Hali
ya Hewa nchini unaonyesha kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha hadi Mei
20 mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kutotupa taka hovyo na kufanyia
usafi mifereji katika maeneo yao.
“Badala ya kulalamika na kuhoji nani wa kulaumiwa kutokana na mafuriko
yanayojirudia jiji la Dar es Salaam, ni jambo la busara sasa kwa kila
mwananchi kuwajibika katika nafasi yake katika kuzuia au kupunguza
kutokea kwa mafuriko hayo” alisema Issa.
Kwa upande wake Afisa Habari wa ForumCC, Tajiel Urioh Aliwataka
Watanzania kutambua kuwa mvua na mafuriko makubwa yanayoendelea kutokea
Dar es salaam na maeneo mengine yanamahusiano mkubwa na ongezeko la Joto
duniani.
“Watu wanapuuza na kuchukulia mzaha mabadiliko ya tabianchi lakini
wanapaswa kujifunza kutokana na mafuriko haya ambayo mbali na
kusababisha vifo pia yameharibu miundombinu ya barabara, nyumba,
madaraja” alisema Urioh
Tafiti zinaonyesha kuwa joto limeongezeka kwa 0.850C duniani huku kwa
Tanzania Joto likiongezeka kwa 10C tangu mwaka 1961 jambo ambalo
linasababisha baadhi ya maeneo kupata mvua zinazozidi kiwango na kuwa na
majanga kama vile mafuriko, vimbunga na ukame.
Hata hivyo, repoti ya Jopo la wanasayansi duniani (IPCC 2007)
inaonyesha, ili kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na mafuriko,
inategemea sana na mipango thabiti ya mipango miji, jinsi ya kutumia
ardhi, ubora wa kuweza kutabiri kutokea kwa mafuriko, utoaji taarifa na
jinsi ya kuchukua hatua.
Mafuriko ya namna hii yaliyoleta athari kubwa ni yale yaliyotokea mwaka
2011 katika Jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu arobaini
(40) huku yakiharibu vibaya miundo mbinu ya barabara, madaraja na makzi
ya watu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni