Mnamo 13 mwezi May
jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa
Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.
Lakini
msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi
mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka. 16.20pm-Nurunziza awasili Bujumbura
Rais Pierre Nkurunziza amewasili katika makao ya rais mjini Bujumbura kupitia msafara mkubwa wa magari .Alikaribishwa na umati mkubwa wa wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamevaa mavazi ya bendera za chama hicho huku wakicheza densi.
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba ametuma picha za wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza kufuatia kuwasili kwa rais huyo katika ,mji mkuu wa Bujumbura
Mashahidi wameiambia BBC kwamba
rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na
amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia
wamemlaki kwa shangwe na vigelegele
Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga
jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa
jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais
Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha
BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa
nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa
poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo
,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna
mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa
wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la
jeshi'',alisema..
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali
Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na
wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.
Source:- BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni