Majambazi hao wakiwa wametiwa pingu baada ya kukamatwa na jeshi la Polisi jijini Dar.
Wananchi wakiwa eneo la Benki ya NMB Sinza-Mori, Dar wakifuatilia tukio
hilo. Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi
wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo
Sinza-Mori, Dar es Salaam.Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika
Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao
walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni