Wiki iliyopita kulikuwa na vichwa vya habari kuhusu Baraza la Sanaa Taifa kutoa barua ya Onyo kwa msanii Shilole baada
ya kuonekana akiwa wazi sehemu za juu ya mwili wake jukwaani kwa bahati
mbaya kwenye show yake aliyoenda kuifanya Ubelgiji.
Shilole na Snura ni watu ambao wanafananishwa na kupambanishwa na wakati mwingine kulinganishwa kwenye muziki wanaoufanya.. Snura amezungumza kuhusu ishu iliyomtokeaShilole.
Snura ameanza
hivi>>’Kiukweli kabla sijataka kusema itakuaje, mimi binafsi
kutoka kwenye moyo wangu namuombea sana msamaha na Watanzania
wasimuangalie hivyo ambavyo wanamuangalia‘
Sentensi nyingine Snura amesema>>’Ile
ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu
mzima na ana maumivu yake ndani ya moyo kwa hiyo unapozidi kumkandamiza
ni kama unazidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona je itatokea
tena?‘
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni