Waziri
wa Kilimo Chakula na Ushirika, ambae pia ni Mbunge wa Bunda mkoani Mara,
Steven Masato Wasira leo ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais kwa
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyikia
baadae mwaka huu.
Wasira
ametangaza siku moja baada ya Kada wa CCM na Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kuliteka jiji la Arusha wakati
akitangaza nia kama hiyo.
Miongoni
mwa makada wa CCM ambao wanatarajiwa kutangaza nia kama ya Lowassa na
Wassira ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba atakae tangaza nia
hiyo baade leo, Charles Makongoro Nyerere, Lazaro Nyalandu, Bernard
Membe, na makada wengine wengi wa chama hicho wametajwa kuwania nafasi
hiyo.
Wasira akitangaza nia hiyo hii leo katika Ukumbi wa BOT jijini Mwanza amesema yeye kauli mbiu yake ni Uadilifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni