Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimefungua milango kwa wanachama wake wenye
sifa za uongozi kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Udiwani, Ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu
wa mwaka huu 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.
Willibrod Slaa amesema, mwanachama aliye tayari ajitokeze kuchukua fomu hizo.Kwa kuzingatia makubaliano ya ushirikiano wao na vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, ratiba ya CHADEMA imejikita zaidi katika kata na majimbo ambayo hawana wawakilishi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni